ccvv
Ndege ya kijeshi ya Marekani aina ya C-130 Hercules iliyoanguka.ccvvb
Ramani inayoonesha eneo ambapo ndege hiyo ilipata ajali.ccvvf
Ndege ya kijeshi ya Marekani aina ya C-130 Hercules imeanguka usiku wa leo katika Uwanja wa Ndege wa Jalalabad nchini Afghanistan na kuua watu 12.
Kanali wa jeshi la Marekani Brian Tribus ameiambia AFP kwamba watao kati ya waliokufa walikuwa wanajeshi wa Marekani, watano walikuwa raia wa kawaida na wawili walikuwa ni Waafghan.

Msemaji wa kundi la wapiganaji la Taliban, Zabihullah Mujahid alisema kupitia Twitter kwamba kundi hilo lilitungua ndege hiyo, lakini mashirika ya habari yanasema hakuna ishara inayoonesha ndege hiyo kama ilishambuliwa.

Jeshi la Marekani limesema linachunguza kilichosababisha ajali hiyo.
Ajali hiyo ya ndege imetokea huku ndege za kijeshi za Marekani zikisaidiana na wanajeshi wa Afghanistan kujaribu kukomboa mji wa Kunduz uliotekwa na wapiganaji wa Taliban.

Takriban wanajeshi 10,000 wa Marekani wamo Afghanistan baada ya mpango wa kuondoa majeshi hayo asteaste kubadilishwa mapema mwaka huu.

Rais Obama alikuwa ameahidi kuacha wanajeshi wachache sana wa Marekani nchini humo ambao wangekuwa wa kulinda ubalozi wa Marekani kufikia mwisho wa mwaka 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...