Mgombea Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli ukihutubia maelfu ya wananchi wa kijiji cha Nkome,Geita Vijijini Mkoani Geita kwenye mkutano wa kampeni,Dk. John Pombe Magufuli aliomba kura za ndiyo kwa wananchi ili wamchague na kuwa rais wa Tanzania  katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini kote ukishirikisha vyama vingi vya siasa


Dk Magufuli akiwahutubia wananchi hao  ambao wengi wao ni wavuvi. amewaomba kutofanya uvuvi haramu kwani unasababisha kuua samaki na mayai yake jambo ambalo linapunguza samaki ziwani na kuwafanya wakose biashara lakini pia watakosa kitoweo.

Ameongeza kwamba Sangara mmoja anataga mayai zaidi ya milioni moja au milioni moja na laki tano, ukiua sangara kumi kwa bomu ni sawa na kuua samaki milioni kumi au kumi na tano ambao wangezaliwa jambo ambalo ni hasara kubwa kwa maliasili zetu za Samaki.

“Ninawaomba kura Ndugu zangu lakini lazima niwe mkweli na msema kweli ni mpezi wa Mungu,  wavuvi wachache wanaofanya uvuvi haramu watubu na kuacha kazi hiyo. Kwani serikali yangu itaongozwa kwa kufuata sheria na Busara ya hali ya juu ili kuwafanya watanzania hasa wa maisha ya kawaida waone faida ya maliasili zao”.
 Wakazi wa mji wa Nkome wakishangilia wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwaomba kura wanachi hao kwenye mkutano wa kampeni,Geita Vijijini
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wananchi wa Geita Vijijini (hawapo pichani) kwenye mkutano wa kampeni uliofanyanika katika kijiji cha Nkome mkoani Geita.
Sehemu ya umati wa watu uliofika kwenye mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli jioni ya leo Geita vijijini 
 Mgombea wa Urais Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli  akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Geita vijijini Ndugu Joseph Kasheku Msukuma katikati katika mkutano wa kampeni uliofanyika mji wa Nkome Geita vijijini. 
 Baadhi ya wakazi wa Geita Vijijini wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli alipokuwa akiwasalimia wakati akielekea mjini Geita mara baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni.

PICHA NA MICHUZI JR-GEITA VIJIJINI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Chagua CCM, chama chenye misingi inayoeleweka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...