Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akiongea na Waheshimiwa Mabalozi wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali na Wakuu wa Idara/Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje. Wengine katika picha hiyo ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Liberata Mulamula. Waziri Membe aliwataka Mabalozi hao kuhakikisha kuwa mafanikio ya kidiplomasia ambayo Serikali ya awamu ya nne imeyapata yanadumishwa na kuendelezwa katika kiwango cha juu zaidi. picha nyingine ni Waheshimiwa Mabalozi waliohudhuria kikao hicho.
Waheshimiwa Mabalozi waliohudhuria kikao hicho
Mhe. Membe akipokea  zawadi ya ramani inayoonesha mandhari mbalimbali za nchi ya Japan. Zawadi hiyo alikabidhiwa na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mhe. Batilda S. Burian.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...