Waziri Mkuu wa zamani Kenya Raila Odinga amempongeza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli baada yake kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Urais Tanzania.
Akiongea katika mahojiano na BBC, Mhe Odinga amemshauri mgombea wa upinzani Mhe. Edward Lowassa Kuwa Kama Hajakubaliana na Matokeo basi Aende Mahakama kushtaki Kama yeye Alivyofanya wakati akigombea Urais Kenya na kushindwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Ameeleza pia matumaini yake kwamba Dkt. Magufuli atahakikisha kuendelea kwa uhusiano mzuri uliopo katia ya Tanzania na Kenya, na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuendeleza ndoto ya kuelekea kwenye Shirikisho la nchi hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Odinga na Magufuli ni marafiki sana!! Marafiki wa karibu mmno!!!

    ReplyDelete
  2. Asante muheshimiwa Raila kwa ushauri muafaka kabisa. Upinzani unajukumu kubwa la kuhakikisha serikali ya awamu ya tano inatimiza wajibu wake kufuatana na taratibu zilizopo. Wajipange kufanya kazi hiyo muhimu.

    Asante jirani zetu Kenya kutuunga mkono katika kipindi hiki. Wakati tunaposhukuru Mungu alivyotuvusha salama tunaimba na wasanii wetu wa hapa nchini,Tukumbuke wasanii wa Kenya wanaoimba Kiswahili kama mama mkenya Jemimah Wa Thiongo na wimbo wake ...AKISEMA ATAKUBARIKI HAKUNA ATAKAYEZUIA .. wimbo wa Mungu ni wa Baraka uko kwenye mtandao. Asante wakenya

    ReplyDelete
  3. Huwezi kwenda mahakamani kushtaki mara Tume ikishamtangaza mshindi. Uchaguzi umeshaisha tufanye kazi. Hujapata hata theluthi moja ya wabunge utakuwa umeshinda kwa kura zipi? Tujenge utamaduni wa kukubali kushindwa na kuacha visingizio.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...