Waziri Mkuu wa zamani Kenya Raila Odinga amempongeza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli baada yake kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Urais Tanzania.
Akiongea katika mahojiano na BBC, Mhe Odinga amemshauri mgombea wa upinzani Mhe. Edward Lowassa Kuwa Kama Hajakubaliana na Matokeo basi Aende Mahakama kushtaki Kama yeye Alivyofanya wakati akigombea Urais Kenya na kushindwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Ameeleza pia matumaini yake kwamba Dkt. Magufuli atahakikisha kuendelea kwa uhusiano mzuri uliopo katia ya Tanzania na Kenya, na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuendeleza ndoto ya kuelekea kwenye Shirikisho la nchi hizo.
Odinga na Magufuli ni marafiki sana!! Marafiki wa karibu mmno!!!
ReplyDeleteAsante muheshimiwa Raila kwa ushauri muafaka kabisa. Upinzani unajukumu kubwa la kuhakikisha serikali ya awamu ya tano inatimiza wajibu wake kufuatana na taratibu zilizopo. Wajipange kufanya kazi hiyo muhimu.
ReplyDeleteAsante jirani zetu Kenya kutuunga mkono katika kipindi hiki. Wakati tunaposhukuru Mungu alivyotuvusha salama tunaimba na wasanii wetu wa hapa nchini,Tukumbuke wasanii wa Kenya wanaoimba Kiswahili kama mama mkenya Jemimah Wa Thiongo na wimbo wake ...AKISEMA ATAKUBARIKI HAKUNA ATAKAYEZUIA .. wimbo wa Mungu ni wa Baraka uko kwenye mtandao. Asante wakenya
Huwezi kwenda mahakamani kushtaki mara Tume ikishamtangaza mshindi. Uchaguzi umeshaisha tufanye kazi. Hujapata hata theluthi moja ya wabunge utakuwa umeshinda kwa kura zipi? Tujenge utamaduni wa kukubali kushindwa na kuacha visingizio.
ReplyDelete