Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Felipe Jacinto Nyusi  wa Msumbiji wakigonga glasi ya kutakiana heri wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake katika ikulu ya nchi hiyo jijini Maputo maarufu kama Ponta Vermelha usiku wa kuamkia leo.Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuwaaga wananchi wa Msumbiji akisisitiza kuwa uhusiano wa kidugu na kipekee kati ya nchi hizo mbili utaendelea kudumu na kukua
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Felipe Jacinto Nyusi wakisimama wakati nyimbo za Taifa zikipigwa wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na ujumbe wake katika ikulu ya nchi hiyo maarufu kama Ponta Vermelha usiku wa kuamkia leo.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Maputo Mh.David Simango akimvisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete vazi maalum na kumkabidhi Ufunguo wa jiji la Maputo kama ishara ya kumtunuku ukazi wa kudumu wa heshima wa jiji hilo wakati wa hafla iliyofanyika katika Jumba la Halmashauri ya jiji la Maputo

 Mstahiki Meya wa Jiji la Maputo Mh.David Simango akijiandaa kumpa  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete  Ufunguo wa jiji la Maputo kama ishara ya kumtunuku ukazi wa kudumu wa heshima wa jiji hilo wakati wa hafla iliyofanyika katika Jumba la Halmashauri ya jiji la Maputo.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Mh Rais Kikwete ni kiongozi mzuri na alikuwa na nia njema sana na nchi yetu tz ila mfumo CCM ulimkwamisha na kumzuia kuyafanya mema mengi aliyokuwa nayo. Nchi nyingi za nje zimenufaika na wingi wa hekima aliyonayo mh. Rais.

    Mh. Rais Mwenyezi Mungu na azidi kukubariki na kukuzidisha katika maisha yako. Uzidi kuwa hazina ya hekima kwa Africa yote.

    mdau
    Texas

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...