Mwakilishi wa Jundokan So Honbu Tanzania, sensei Fundi, 3rd Dan (pichani chini), mwenye makaazi yake Marekani, amealikwa kushiriki moja ya semina ( Gasshuku) ya Karate mtindo wa Okinawa Goju Ryu Karate-Do Jundokan So Honbu. 

Semina hii itafanyika nji wa Leeds, Uingereza, kuanzia tarehe 16 hadi 18 Oktoba, 2015. 
Wakuu wa Jundokan toka visiwa vya Okinawa wakiwemo; Sensei Yoshihiro Miyazato, Kancho ambae ni mtoto wa mwanzilishi wa Jundokan dojo mwaka 1957 master Eiichi Miyazato ( aliyekuwa mwalimu wa Sensei Bomani toka mwaka 1968), ndie mwenyekiti wa sasa wa Jundokan So Honbu Dojo na ataongoza wajumbe toka Okinawa, ambao ni; Sensei Tsuneo Kinjo 9 Dan, Gima Sensei 9 Dan, Sensei Yurio Nakada 9 Dan na masensei wakuu wa Jundokan matawi ya Ulaya yote. 
Sensei Fundi, atakuwa Mtanzania pekee kuwakilisha tawi la Tanzania. Pia, Sensei Fundi, alipata fursa ya kuwa na wakuu hao mwezi wa Juni mwaka huu alipotembelea visiwani Okinawa, katika mji wa Naha. Mbinu za Karate, Kata Bunkai ( Tafsiri za kutumia mbinu za mapambano za kujilinda) na maendeleo yake duniani ni moja ya mambo yatakayo jadiliwa katika semina hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Yahya SamejaOctober 06, 2015

    Hongera Sensei Rumadha kwa kutuwakilisha waTanzania katika Semina ya Okinawa Goju Ryu Karate-Do Jundokan So Honbu huko Leeds.

    Way to go Sensei

    ReplyDelete
  2. Sensei Rumadha Fundi unakubalika kimataifa ,hongera sana kwa kuipeperusha bendera ya TZ kimataifa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...