Serikali ya Kenya na watu wake wameelezea shukrani zake kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa urafiki na ushirikiano thabiti aliouonyesha kwa watu wa Kenya katika kipindi cha miaka 10 ya uongozi wake. 
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema hayo tarehe 5 Oktoba, 2015 katika Ikulu ya Nairobi wakati wa mazungumzo ya kiserikali.
 "I thank you, and on behalf of People of Kenya for your friendship and Cooperation that was reflected during your 10 years as President" Rais Kenyatta amemueleza Rais Kikwete wakati wa mazungumzo yao jijini Nairobi. 
 "Chini ya uongozi wako Kenya na Tanzania zimeongeza ushirikiano baina yao katika miundombinu, biashara, uwekezaji, sekta binafsi na biashara ambapo imeongezeka na kuifanya Tanzania kuwa soko kubwa la Kenya" Rais Uhuru amesema. 
 Rais Kikwete yuko nchini Kenya kwa Ziara ya kiserikali ya siku tatu, ambapo pamoja na mambo mengine , Rais Kikwete atahutubia Bunge la Kenya na kukutana na wafanyabiashara wa nchini Kenya. 
 Mara baada ya kuwasili jumapili jioni Rais Kikwete alikutana na Watanzania waishio nchini Kenya na kula nao chakula cha usiku katika Hoteli ya Villa Rosa Kempisky. 
Watanzania hao wamemshukuru Rais na kumpongeza kwa mafanikio yanayoshuhudiwa nchini. Akisoma risala yao Makamu mwenyekiti wa umoja wa Watanzania waishio nchini Kenya, Bw Cleophas Tesha amesema mafanikio hayo yametokana na juhudi binafsi za Rais Kikwete na Serikali ambayo ameisimamia kwa miaka yote 10. 
 "Kwa Umakini wako katika kusimamia maslahi ya wananchi, uimara wako bila kushinikizwa, tunakupongeza kwa kuweka nchi yetu katika ramani ya dunia". Amesema Bw. Tesha "Tunaamini bado Taifa litaendelea kutumia ujuzi wako". 
Leo Usiku Rais Kikwete na ujumbe wake wamehudhuria dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima yake. Kesho tarehe 6 Rais Kikwete anatarajia kuhutubia Bunge la Kenya na wananchi wake ambapo anatarajia kuwaaga rasmi Rais Kikwete na ujumbe wake wanatarajia kuondoka Nairobi kurudi Dar-es-Salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Nairobi leo Jumatatu October 5, 2015 alipokwenda kwa mapokezi rasmi ya ziara yake pamoja na mazungumzo na hatimaye kuaga.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kwa Mkuu wa Majeshi ya Kenya Jenerali Samson Mwathete katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Nairobi leo Jumatatu October 5, 2015 alipokwenda kwa mapokezi rasmi ya ziara yake pamoja na mazungumzo na hatimaye kuaga.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akisalimiana n viongozi mbalimbali katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Nairobi leo Jumatatu October 5, 2015 alipokwenda kwa mapokezi rasmi ya ziara yake pamoja na mazungumzo na hatimaye kuaga.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Amos Makalla kwa  mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akisalimiana n viongozi mbalimbali katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Nairobi leo Jumatatu October 5, 2015 alipokwenda kwa mapokezi rasmi ya ziara yake pamoja na mazungumzo na hatimaye kuaga
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima  katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Nairobi leo Jumatatu October 5, 2015 alipokwenda kwa mapokezi rasmi ya ziara yake pamoja na mazungumzo na hatimaye kuaga.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katik mazungumzo ya tete-a-tete  katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Nairobi leo Jumatatu October 5, 2015 alipokwenda kwa mapokezi rasmi ya ziara yake pamoja na mazungumzo na hatimaye kuaga. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...