NA MWANDISHI WETU WASHINGTON 
SERIKALI ya Tanzania imetakiwa kuhakikisha kuwa amani na usalama vinakuwepo wakati na baada ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini Tanzania tarehe 25 mwezi huu.
Profesa Nicholas Boaz,
Wito huo umetolewa na Mhadhiri wa Mawasiliano na Sera katika Chuo Kikuu cha Maryland nchini Marekani, Profesa Nicholas Boaz katika mahojiano maalum na Swahilivilla.

Akizungumza na mwandishi wetu nyumbani kwake, Profesa Boaz ambaye amerejea nchini Marekani hivi karibuni baada ya ziara yake Tanzania, alisema kuwa nchini Tanzania kuna joto kali sana na vuguvugu la mabadiliko."Kuna joto kali sana la uchaguzi. Kwa kweli naona watu wengi wanaitikia wito wa kutaka mabadiliko", alisistiza profesa Boaz.

Alisema kuwa hali duni za wananchi katika nyanja mbalimbali za maisha baada ya miaka mingi ya utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na miaka kumi ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete, ndiyo iliyopelekea mwamko wa vuguvugu la kutaka mabadiliko. 

"Baada ya muda mrefu wa CCM kuwa madarakani, na miaka kumi ya Rais Kikwete, basi watu wamepata mwamko kuwa maisha na maendeleo yao yamekuwa duni.

 Kwa hivyo wanataka wapate mabadiliko ya kiongozi na kimtazamo juu ya namna ya kuweza kuwasaidia watu hasa katika maswala ya kazi, afya, mamno ya shule na mambo mengine mengi".

Aliyataja mambo hayo mengine kuwa ni swala la uhuru wa watu kujieleza na kuuliza juu ya kitu ambacho kinawakera.

Akijibu swali iwapo kweli wananchi wa Tanzania wamepata mwamko wa mabadiliko au wanaimba tu nyimbo za wanasiasa, Bwana Boaz alisema "Huwezi kuingia akilini mwa watu kuwajua nini wanakitaka. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Anayechezea amani ya nchi ni mtu ambaye hatutakii mema. Mtanzania mwenye akili hawezi kupigana au kuharibu mali ya wengine kwa sababu ya uchaguzi. Tuzingatia amani wakati wote hakuna sababu ya kuwepo kwa vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani, usipofanikiwa uchaguzi huu, fanya kazi nyingine ukingoja kujaribu uchaguzi ujao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...