
Serikali
imetoa ufafanuzi kuhusu ukomo wa madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na mwisho wa uhai wa Baraza la Mawaziri kwa kadri Tanzania
inavyoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaofanyika Jumapili, Oktoba 25, mwaka huu,
2015.
Taarifa
iliyotolewa jioni ya leo, Jumatano, Oktoba 21, 2015, Ikulu, Dar es Salaam na Ofisi
ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Yohana Sefue imesema kuwa Serikali imetoa
ufafanuzi huo kuwasaidia wananchi kuelewa maelekezo na matakwa ya Katiba na Sheria
kuhusu ukomo wa madaraka ya Rais na mwisho wa Baraza la Mawaziri kufuatia mijadala
ya karibu katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
Taarifa
hiyo imekariri Ibara ya 42(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
1977 ambayo inasema kuwa ukiacha sababu nyingine, mtu anayechaguliwa kuwa Rais atashika
madaraka ya kiti cha Urais hadi Rais Mteule atakapoapishwa.
Ibara
hiyo ya 42(3) inasema: ”Mtu anayechaguliwa kuwa Rais, atashika kiti
cha Rais hadi – (a) siku ambako mtu anayemfuatia katika kushika kiti hicho atakula
kiapo cha Rais.”
Taarifa
hiyo imesema: “Hivyo, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais anaendelea
kuwa Rais, akiwa na madaraka na mamlaka yote na kamili yanayoambatana na nafasi
hiyo, hadi Rais Mteule anakapokula kiapo cha Urais. Hivyo, ni vyema wananchi waelewe
kuwa hakutatokea wakati wowote ambapo hakuna Rais na Amiri Jeshi Mkuu mwenye mamlaka
kamili na aliye tayari kuyatekeleza mamlaka hayo. Lengo ni kuhakikisha kuwa haitokei
wakati wowote nchi yetu ikakosa Rais na Amiri Jeshi Mkuu.”
Imesisitiza
taarifa hiyo: “Madaraka na mamlaka ya Rais yapo, na hayapugui kwa namna yoyote ile,
hata baada ya Uchaguzi Mkuu, mpaka Rais Mteule atakapoapishwa.”
Kuhusu
ukomo wa Baraza la Mawaziri, taarifa imefafanua kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 57(2) ya Katiba, Waziri na NaibuWaziri ataendelea
kushikilia mamlaka ya nafasi yake hadi, ukiacha sababu nyingine, Rais mteule atakapoapishwa.
Ibara hiyo 57(2) inatamka: “Kiti
cha Waziri au NaibuWaziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo
– (f) Ukiwadia wakati wa Rais Mteule kushika madaraka ya Rais, basi mara tu kabla
ya Rais Mteule hajashika madaraka hayo.”
Taarifa
hiyo imeongeza kuwa Mawaziri na NaibuMawaziri wanaendelea kushikilia nafasi zao,
wakiwa na madaraka na mamlaka kamili yanayoambatana na nyadhifa zao hadi mara tu
kabla ya Rais Mteule hajashika madaraka.
Imemalizia
taarifa hiyo: “ Naomba vyombo vya habari, vyenye jukumu la kuelimisha jamii, kuwaelewesha
Watanzania kuhusu utaratibu huu wakubadilishana madaraka kati ya awamu moja ya uongozi
wa nchi na nyingine. Madaraka na mamlaka ya Rais yapo, na hayapungui kwa namna yoyote
ile, hata baada ya uchaguzi Mkuu mpaka Rais Mteule atakapoapishwa.”
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
21 Oktoba, 2015


Nashukuru kwa Kurugenzi kutoa maelekezo ya Ukomo wa Urais na Uwaziri hapa nchini. Mtoa maelezo asipotoe katiba kulinda makosa ya kimakusudi na kwa makusudi kwani ni bora angekaa kimya kuliko kupotosha ukweli hali uko wazi.
ReplyDelete1. Kuhusu Rais ni sawa kabisa nakubaliana na maelezo yake; isipokuwa sehemu ya kuwa bado ni Amiri Jeshi mkuu hadi sasa wakati majeshi yalishamuaga hivyo kwao ni kama Raia yeyote wa Tanzania si Amiri jeshi tena.
2.Pili kifungu cha sheria alicho nukuu 57 (2) aelezee kifungu B na E kinachoelezea kuwa waziri na Naibu waziri wanakoma mara tu Bunge linapovunjwa maana sifa mojawapo ya mtu kuwa waziri ni kuwa MB wa Tanzania. Kwanini anaruka vifungu hivyo vinavyoonyeshwa kukiukwa kimakusudi? Nafikiri Tanzania ya sasa ni ya wanaoona ni bora msemaji huyu akae kimya kuliko kuongeza hasira za watu bila sababu.Kama anamaanisha basi atoe maelekezo ya vifungu nilivyonukuu kama vinahalalisha mawaziri kuendelea na kazi zao hadi sasa!
Keep going Michuzi Blog...
Michael Mwasumbwe
Huu ni utaratibu wa kawaida nchi nyiingine hata baada ya kutangazwa mshindi kuna kuwa na wiki tatu za kukabidhiana madaraka na kumwezesha kiongozi mpya kuunda baraza la mawaziri na timu yake kuanza kazi. Hakuna vacuum inayoruhusiwa wakati wanaokuja wanapojipanga.
ReplyDelete