Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo (kulia) na Mkuu wa ofisi ndogo ya Umoja wa Mataifa Zanzibar, Anna Senga (katikati) wakimkaribisha mmoja wa wageni waalikwa katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
SERIKALI ya mapinduzi Zanzibar imesema kuwa itaendelea kuthamini fursa mbali mbali zinazotolewa na Umoja wa Mataifa (UN) ili ziweze kuwanufaisha wananchi wote bila ya ubaguzi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma, Haroun Ali Suleiman wakati akihutubia katika sherehe za kutimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Shangani Mjini Zanzibar, alisema umoja huo umekuwa sekta muhimu ya kuunga mkono juhudi za maendeleo ya serikali katika sekta mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Alisema kuwa Zanzibar ikiwa miongozi mwa nchi zinazoendelea barani Afrika inaendelea kutumia vizuri fursa zinazotolewa na umoja huo kwa lengo la kujenga jamii bora zenye kipato na uwezo wa kati kwa lengo la kupunguza umasikini nchini.
Waziri Haroun alifahamisha kuwa miradi mbali mbali ya maendeleo inayotolewa na umoja huo imekuwa nyenzo muhimu ya kuisaidia serikali kuhudumia wananchi wake kwa ufanisi zaidi.
Alisema kutokana na misaada hiyo Zanzibar pia imekuwa mdau muhimu wa umoja huo kwani ni miongoni mwa nchi yenye urithi wa kimataifa kupitia maeneo ya Mji Mkongwe jambo ambalo ni ishara tosha ya mahusiano mema kati ya umoja huo na serikali.
Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa visiwani Zanzibar wakibadilishana mawazo wakati wa kuwasili kwa wageni waalikwa kwenye sherehe hizo.
“ Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inajali kwa kiasi kikubwa juhudi za Umoja wa Mataifa kwa kutuunga mkono, nasi tunaendelea kutumia vizuri miradi mnayotuunga mkono.
Pia tunaendelea kukuombeni mtusaidie pale tutakapohitaji msaada wenu kwa Nyanja tofauti kwani bajeti ya serikali haitoshi kukidhi mahitaji yote ya kuendesha serikali.”, Alisema Waziri Haroun.
Naye Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez alikiri kuridhishwa kwake na utekelezaji wa miradi mbali mbali ya umoja huo na kuahidi kuendelea kushirikiana vizuri na serikali ili kufikia dhana ya maendeleo endelevu Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.
Bw. Rodriguez alibainisha kuwa umoja huo bado unaendelea kufanya tathimini na utafti juu ya masuala mbali ya kisiasa na kijamii nchini ili kuona ni kwa jinsi gani watasaidia kuunga mkono maeneo hayo kwa maendeleo ya nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...