Mawaziri  wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona siku walipohukumiwa kifungo cha miaka mitatu na faini ya milioni tano baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka Mwezi Julai mwaka huu. Picha ya maktaba
Na Mwene Said wa 
Blogu ya Jamii, Dar es Salaam.
 MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kesho imepanga kutoa hukumu ya rufaa dhidi ya mawaziri  wa zamani, Bazil Mramba na Daniel Yona waliohukumiwa kifungo cha miaka mitatu na faini ya milioni tano baada ya kukutwa na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka. 
Mapema Agosti 5, mwaka huu mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Projest Rugazia iliagiza pande zote mbili kuwasilisha hoja za kusikiliza rufaa hizo kwa njia ya maandishi. 
Upande wa Jamhuri ulikata rufaa Mahakama Kuu kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumwachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja, kwamba ushahidi uliotolewa haukuthibitisha makosa dhidi ya tuhuma za  matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.
 Kadhalika, Mramba na Yona walikata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa dhidi yao na jaji alipanga kutoa hukumu Septemba 18, mwaka huu lakini alipata maradhi akaahirisha hadi leo. 
Jaji Rugazia atasoma hukumu ya kuwaachia ama kukazia hukumu ya Mahakama ya Kisutu kesho. 
Wafungwa hao kwa pamoja wamekutwa na hatia ya makosa ya kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation kwa ajili  ya kufanya ukaguzi wa madini ya dhahabu nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hawa wezi si walishapigwa mvua ni nini tena ???? na mkithubutu kuwaachia basi mjue hamna chenu october!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...