Asakari polisi na wataalamu wakikagua mabaki ya chopa namba 5Y-DKK iliyoanguka jana jioni ikitokea Dar kuelekea Ludewa sehemu ya hifadhi ya wanyama ya Selous ambapo Mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe, rubani Capt. William Slaa na abiria wengine wawili - Casablanca Haule na Ngondombwitu Nkwera - walipoteza maisha.
Timu ya waokoaji wakibeba mabaki ya miili ya marehemu
Askari wakiwa eneo la ajali


Mbunge wa Ludewa Mhe Deogratias Haule Filikunjombe (chini) amefariki dunia katia ajali ya Chopa katika hifadhi ya wanyama ya Selous, pamoja na rubani Kepteni William Silaa (juu kulia), mfanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa na ndugu yake Marehemu Filikunjombe ambao majina hayajapatikana mara moja.
Mhe. Deo Filikunjombe, rubani na na abiria wengine walipata matatizo ya engine ya chopa namba 5Y-DKK jana jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa.
Kwa mujibu wa Meya wa Ilala aliyemaliza muda wake Mhe Jerry Silaa, ambaye ni mtoto wa rubani, hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo ya Chopa.
"Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji kuwa imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha.
"Ni mepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt. William Silaa. Nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe. Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amani. Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi", amesema Mhe Jerry Silaa katika kurasa zake za mitandaoni.
tangia jana habari za kuanguka kwa nchopa hiyo zilitapakaa kila kona na katika mitandao, na kuendelea hadi leo tangia asubuhi hadi baada ya ujumbe wa Jerry Silaa kupatikana mchana huu.
Hoooo nakulilia Filikunjombe jembe letuuu. Mungu tuhurumie siye pamoja na nchi yetu ni nini hiki mungu, hatupumziki !!!!! RIP Deo we always remember you.
ReplyDeleteJamani ni huzuni kubwa,pumzikeni kwa amani wote,poleni wafiwa.Ankal huyu Rubani namfananisha na Rubani Fulani alikuwa anarusha Chopa mjini Geita mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwenye masuala ya uchimbaji madini na alijengea hoteli/"kiwanja" kimoja maarufu sana Geita Enzi hizo kinaitwa Lake View kama sikosei.Alikuwa mpole na mkarimu sana tulimpenda.
ReplyDeleteDavid V
Poleni wafiwa. Mungu awatie nguvu wakati huu mnapoomboleza kwa kupotelewa na wapendwa wenu. Matumizi ya chopa nayo yapunguzwe mpaka zitakapokuwa katika hali ya usalama.
ReplyDeleteDaa inasikitisha sana
ReplyDeleteRIP na pollen wafiwa
ReplyDeleteR.I.P Mpiganaji Deo Filikunjombe
ReplyDeleteMungu azilaze roho za Marehemu mahali pema. Jamiani hizi picha zinasikitisha. Sielewi kusoma kuwa timu ya uokoaji wakati sioni hawajajiandaa kwa hali yeyote. Mavazi, vifaa vya uokoaji na kujikinga na maambukizi yeyote. Hata machela naona kuwa ilikatwa miti ya mahali hapo. Jamani hii hali inasikitisha sana.
ReplyDeleteKwa kweli Mungu atubariki na ccm yetu. Hii miili ililala huko huko pirini. Kweli tuko nyuma kupita kiasi. Wapumzike kwa Amani.
ReplyDeleteWé lost a courageous guy who fought for his people.
ReplyDeleteRip deo platun leader CCP moshi 1999/2000
ReplyDeleteDeo ni kijana ambae siku zote alisimamia na kulitetea Taifa la Tanzania kwa nguvu zake zote bila ya kujali kwamba itikadi ya chama chake kinasemaje.
ReplyDeleteTanzania imempoteza mtu muhimu sana; Nani atakuwepo kulitetea Taifa? Kwanini watetezi wa Taifa wanafariki sana? Nakuomba Mungu utuwekee hai watetezi waliobakia na kutuletea wengi zaidi.
Nakuomba Mwenyezi Mungu uilaze roho ya marehemu Deo mahali pema peponi amin; Msamehe makosa na dhambi zake alizozifanya hapa duniani na huko mbinguni na siku ya mwisho nakuomba mkumbuke katika ufalme wako wa mbinguni.
Tanzania idumu daima; Muungano udumu daima! Mungu ibariki Tanzania na watu wake.
Asanteni.
Rest in peace Mbunge wetu, Mh. Deo Filikunjombe (Haule).
ReplyDeleteRIP DEO
ReplyDelete