JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.

       TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
   “PRESS RELEASE” TAREHE 09.10.2015.

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA BAADA YA GARI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 440 AXX AINA YA MITSUBISHI CANTER IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE PWELA MWALEMBO (30) MKAZI WA ILEMBO LILILOKUWA LIKITOKEA KIJIJI CHA ITUMBA WILAYA YA ILEJE KUELEKEA ITALE ILIACHA NJIA NA KUPINDUKA.
WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO NI 1. IMANI MBEYALE (27) NA 2. IYELA SAID (33) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ITALE.

AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 08.10.2015 MAJIRA YA SAA 19:30 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISHENTA, KATA YA NDOLA, TARAFA YA BULAMBYA, WILAYA YA ILEJE, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA ITUMBA/IWIJI.

AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU 23 WALIJERUHIWA KATI YAO WANAUME 20 NA WANAWAKE 03 AMBAO WOTE WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA ILEJE. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA/ALAMA NA MICHORO YA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.

Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...