JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
 WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
 “PRESS RELEASE” TAREHE 12.10.2015.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

MTU MMOJA MKAZI WA NZOVWE JIJINI MBEYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA MALI YA WIZI.

MTU MMOJA MKAZI WA NZOVWE JIJINI MBEYA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA BARAKA SHANSIYA (26) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA  AKIWA NA KIPANDE KIMOJA CHA SHABA MALI AMBAYO NI YA WIZI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.10.2015 MAJIRA YA SAA 05:00 ALFAJIRI HUKO ENEO LA SONGWE – DARAJANI, KATA YA SONGWE, TARAFA YA USONGWE, NJE KIDOGO YA JIJI LA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA.

INADAIWA KUWA, MTUHUMIWA AKIWA NA MWENZAKE WALIIBA VIPANDE VIWILI VYA SHABA KUTOKA NDANI YA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.914 BPA/T.277 DET AINA YA SCANIA BAADA YA KUKATA TURUBAI NA CLAM NA KISHA KUIBA. GARI HILO LILIKUWA LIKITOKEA JIJINI DAR ES SALAAM KUELEKEA NCHINI KONGO NA NDIPO MSINDIKIZAJI WA MIZIGO YA KAMPUNI YA TRIPPLE “A” YA JIJINI DAR ES SALAAM ELIA SANGA (22) MKAZI WA D’SALAAM ALIPOGUNDUA KUIBWA KWA VIPANDE HIVYO NA KUTOA TAARIFA.
BAADA YA TAARIFA HIZO, MSAKO MKALI ULIENDESHWA NA NDIPO MTUHUMIWA ALIKAMATWA AKIWA NA KIPANDE KIMOJA CHA SHABA. THAMANI YA MALI ILIYOIBWA BADO HAIJAFAHAMIKA, UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUKITAFUTA KIPANDE KINGINE AMBACHO BADO KUPATIKANA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO ANATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI LA WIZI ILI WAKAMATWE. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA WA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
                                                            Imesainiwa na:
[NYIGESA R. WANKYO – ACP]

KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...