JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
“PRESS CONFERENCE” TAREHE 23.10.2015.
NDUGU
WAANDISHI WA HABARI,
TUNAJUA KUWA TAREHE 25 OKTOBA, 2015 NI SIKU AMBAYO
TUTASHIRIKI KUPIGA KURA KUWACHAGUA MADIWANI, WABUNGE NA RAIS KWA KIPINDI CHA
MIAKA MITANO IJAYO.
KATIKA KUELEKEA SIKU HIYO, YAPO MAMBO KADHA WA KADHA AMBAYO
KILA MMOJA WETU KWA NAFASI ALIYONAYO ANAPASWA KUYAFUATA NA KUYAZINGATIA KWA
LENGO LA KUHAKIKISHA UCHAGUZI MKUU UNAKUWA HURU NA HAKI.
TUTAMBUE KUWA KILA
MMOJA WETU ALIYEFIKISHA UMRI WA MIAKA 18
NA KUENDELEA NA ALIYEJIANDIKISHA ANA
HAKI YA KUPIGA KURA. NI MUHIMU KUFIKA KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA UKIWA NA
KADI YA MPIGA KURA [SHAHADA YA KUPIGIA KURA] KWA MUJIBU WA TUME YA TAIFA YA
UCHAGUZI VITUO VYA KUPIGIA KURA VITUFUNGULIWA KUANZIA SAA 07:00 ASUBUHI HADI 16:00
JIONI.
KILA
MMOJA AKUMBUKE KUJIEPUSHA KUFIKA KATIKA KITUO CHA KUPIGIA
KURA AKIWA AMEVAA NGUO ZENYE PICHA ZA WAGOMBEA, MANENO AU NEMBO AMA RANGI ZA
CHAMA CHA SIASA, KUEPUKA KUTUMIA
UVUMI, MANENO YA UONGO, HISIA AU VISINGIZIO VYENYE LENGO LA KUWAZUIA WENGINE
KWENDA KUPIGA KURA, KUEPUKA KUFANYA
KAMPENI KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA IWE KWA MANENO YA USHAWISHI AU KWA
KUONYESHA ISHARA YA CHAMA FULANI CHA SIASA.
AIDHA NI VYEMA KILA
MWANANCHI KUPIGA KURA KWA KUTUMIA JINA NA KITAMBULISHO CHAKE NA SIO CHA MTU
MWINGINE, ALIYEKUFA AU MGONJWA, KUEPUKA
KUFANYA FUJO AMA VURUGU KATIKA KITUO CHA KUPIGIA KURA. NI MUHIMU KILA MPIGA
KURA MARA BAADA YA KUPIGA KURA KUONDOKA KWENYE KITUO CHA KUPIGIA KURA NA
KUENDELEA NA SHUGHULI NYINGINE KWANI NI KOSA KUPIGA KURA NA KUENDELEA KUBAKI
KATIKA ENEO LA KITUO CHA KUPIGIA KURA.
AIDHA NI WAJIBU WA
JESHI LA POLISI KUWALINDA MAOFISA WANAOSIMAMIA UCHAGUZI, KUHAKIKISHA KWAMBA
ZOEZI LA UPIGAJI KURA LINAENDA SAWA, BILA VIKWAZO AU BUGHUDHA NA KUHAKIKISHA
VIFAA VYA KUPIGIA KURA VIKO SALAMA.
KWA MKOA WA MBEYA TUNA
JUMLA YA MAJIMBO 13 YA UCHAGUZI, VITUO 3,899 VYA KUPIGIA KURA, KILA
KITUO KITALINDWA NA ASKARI ILI KUHAKIKISHA SUALA LA ULINZI NA USALAMA
LINAIMARISHWA KWA KIPINDI CHOTE CHA ZOEZI LA KUPIGA KURA, KUHESABU KURA NA
KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI.
JESHI LA POLISI MKOA WA
MBEYA LIMEJIPANGA KUIMARISHA ULINZI KATIKA MAENEO YOTE IKIWA NI PAMOJA NA VITUO
VYA KUPIGIA KURA. PIA KUTAKUWA NA DORIA ZA MAGARI, PIKIPIKI, MBWA NA ASKARI
AMBAO WATAKUWA WAKITEMBEA HUKU NA KULE KWA LENGO LA KUDHIBITI VITENDO VYOVYOTE
VYA UVUNJIFU WA AMANI. IELEWEKE KUWA, VITENDO VYOVYOTE VYA UVUNJWAJI WA SHERIA
KABLA, WAKATI NA BAADA YA UCHAGUZI NI UHALIFU HIVYO KILA MMOJA AWE MAKINI NA
AFUATE SHERIA/TARATIBU NA ATIMIZE WAJIBU WAKE WAKATI WOTE.
JESHI LA POLISI
LINAWATAKA WANANCHI WAHESHIMU MAELEKEZO YA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI. KWAMBA
WALE WOTE WATAKAOPIGA KURA NA MARA BAADA YA KUPIGA KURA WAONDOKE MAENEO YA
VITUO VYA KUPIGIA KURA WAENDE KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO, “WASIKUSANYIKE”
WASIWEKE MKUSANYIKO KWANI KWA KUFANYA HIVYO WATAKUWA WANAFANYA MKUSANYIKO USIO
HALALI “UNLAWFUL ASSEMBLY” MKUSANYIKO WOWOTE USIOFUATA UTARATIBU HALALI.
NARUDIA, JESHI LA
POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA DOLA LIMEJIPANGA VIZURI KUIMARISHA ULINZI
NA USALAMA KATIKA MAENEO MBALIMBALI ILI KUHAKIKISHA ZOEZI ZIMA LINAKWENDA
VIZURI, KWA USALAMA NA AMANI NA UTULIVU. KWA HIVYO WANANCHI WOTE WENYE SIFA
WAENDE KUPIGA KURA, WASIOGOPE.
NAOMBA TUELIMISHANE ILI
KUEPUKA MAKOSA AMA UHALIFU, KILA MMOJA ANA WAJIBU WA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA
ULINZI NA USALAMA ILI KUUFANYA UCHAGUZI UWE WENYE AMANI NA UTULIVU, HURU NA
HAKI. NI IMANI YANGU KUWA KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI HIVYO TULINDE NA
KUTETEA AMANI YA NCHI YETU.
AHSANTENI KWA
KUNISIKILIZA!
KATIKA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, MNAMO TAREHE 20.10.2015 MAJIRA YA SAA 14:00 MCHANA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA LILIPOKEA TAARIFA KUWA, MTU MMOJA AITWAYE RAMADHANI JUMA MSUMA @ RAMA BAJAJI (25) MKAZI WA FOREST YA ZAMANI
JIJINI MBEYA, ANATUHUMIWA KWA MAKOSA YA MATUMIZI MABAYA YA MTANDAO KWA KUTUMIA
PICHA ZA KUZALILISHA WAGOMBEA WA VYAMA VYA SIASA NA KUTOA TAARIFA ZA UCHOCHEZI
DHIDI YA VYOMBO VYA DOLA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI, KINYUME NA SHERIA.
NJIA ALIYOKUWA AKITUMIA MTUHUMIWA NI
KUTUMIA NAMBA ZA SIMU ZAKE ZA MKONONI ZILIZOSAJILIWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
@ WHATSAPP, FACEBOOK, INSTRAGRAM NA
TWITTER AMBAPO ALIKUWA AKITENGENEZA PICHA ZA UZALILISHAJI NA TAARIFA ZA
UCHOCHEZI NA KISHA KUZITUMA KWA NJIA YA MTANDAO KATIKA MAKUNDI MBALIMBALI YA
MITANDAO YA KIJAMII TAJWA HAPO JUU.
AIDHA PICHA HIZO NA TAARIFA HIZO ZINATOA
KASHFA KWA WAGOMBEA WA VYAMA VINGINE NA KUTOA VITISHO KWA KUELEKEA UCHAGUZI KWA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI. PIA TAARIFA HIZO NI VIASHIRIA VYA UCHOCHEZI WA
VURUGU/FUJO NA UVUNJIFU WA AMANI NA USALAMA HUSUSANI KATIKA KIPINDI HIKI CHA
UCHAGUZI MKUU.
MTUHUMIWA ANAHOJIWA NA PINDI UPELELEZI
UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI MARA MOJA KUJIBU MASHITAKA YANAYOMKABILI
CHINI YA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO NA.
14 YA 2015.
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA
MTANDAO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA ZA MATUMIZI SALAMA YA MTANDAO ILI
KUJIEPUSHA NA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA
KUELEKEA UCHAGUZI MKUU HAPO OKTOBA 25,
2015.
Imesainiwa na:
[AHMED
Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...