Mwezi Huu wa October, Nimekua na kazi kubwa ya kuhimiza mashirika, makampuni pamoja na Taifa kwa ujumla kuutumia vizuri kutokana na kua ni mwezi maalum uliotengwa na wanausalama mtandao kote duniani wa kukuza uelewa wa matumizi salama ya mitandao ili kuweza kupunguza wimbi kubwa la uhalifu mtandao duniani kote.
Nategemea kuandikia yaliyo jiri Nchini kwetu hapo baadae ili kuweza kujua namna mwezi huu tulifanikiwa kukuza uelewa kupitia mashirika mbali mbali na taifa kwa ujumla wake. Kitu ambacho niliweza kukiwasilisha ndani ya mwezi huu ni Maazimio ya namna ya kukabiliana na uhalifu mtandao katika ngazi ya Taifa, Bara Na Duniani kwa ujumla ambapo ni maazimio tuliyo kubaliana kimsingi tulipo kutanda Mwaka huu mwezi wa Tano Nchini Afrika kusini. Kusoma zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...