Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Uislamu na Chama wapi na wapi. Hiyo ni Dini na hicho ni chama, mithli ya PAKA na MUWA. Sidhani kama kuna kuhusiana kokote mpaka kuwe na kauli kama hiyo ya kuwataka Waislam nchini kuelekeza kura zao huko palipotajwa. Kila mtu ana haki sawa na ana uhuru wa kufanya maamuzi yake anayoyataka, kwa yeyote yule au popote pale na kwa wakati wowote ule, almuradi tu asivunje sheria na taratibu zilizowekwa kwa jambo lolote husika na nchi kwa jumla, tusianze kuwa na vyanzo vidogo vidogo vya kutaka kutuvurugia amani na utulivu tulionao katika nchi yetu, maana kauli kama hivyo ni uchochezi wa chini chini ambao unaofanywa na watu wachache na usipoangaliwa khatma yake unakuja kutuzushia balaa na mvurugano na kujenga tofauti miongoni mwetu na kuharibu amani yetu na utulivu tunaojivunia nchini. Uislam hauna chama, binaadamu ndie mwenye maamuzi yake na ndie anaeweza kuamuwa apende chama gani au mgombea yupi. Waislamu wao ni waumini tu wa imani hiyo, lakini pia ni binaadamu kama wengine, kadhalika mtu ana maamuzi yake na siyo kuhamasisha au kuvumisha kwa kauli ambazo hazipo na wala hazina ithibati yeyote. Uwe Mwislamu, Mkristo, Mpagani, wewe kajipigie kura yako na jichagulie unaemtaka na taratibu jirudie nyumban kwa salama na amanii ukayasubiri matokeo, ambayo naamini hayatakuwa ya Waislam wala wakristo wala wapagani, bali ni matokeo ya USHINDI WA TAIFA ZIMA LA TANZANIA KWA MANUFAA YA WATANZANIA WENYEWE KATIKA NCHI YAO.

    Mungu Ibariki Tanzania, Ibariki Afrika na Ubariki Ulimwengu mzima kwa jumla. Amen!

    ReplyDelete
  2. Umesema wana akili sasa tamko la nini?

    Naona na wewe unawaswaga.

    Pili, kupiga kura hakuvunji amani hata kama ni kwa asiyetakiwa. Ingekuwa kuvunja amani kama hao jamaa wangewashikia silaha na kuwaamuru bali waliwashawishi tuu?

    Jamani mkumbuke uhuru wa kauli. Baraza lina uhuru wa kauli na hao wapinzani wa baraza pia wana haki sawa na baraza. Huu ndo uhuru wa kweli na amani itokanayo na uhuru huu ndo ya kweli. Tusiziwie watu kusema watakalo kama sisi tusivyozuwiliwa. Bali tuna uhuru wa kuona yasemwayo ni mabaya au mazuri.

    Mtu yeyote ana haki ya kumwambia mtu yeyote atakacho ikiwa huyo mtu yeyote ataruhusu. Kama hao wasikilizaji waliruhusu itoshe. Inawezekana anachomwambia ni kibaya au kizuri yeye mwenyewe atajuwa siyo wewe kumwambia ni kibaya. Umeshasema wana akili sasa tamko la nini?

    Msiziwie uhuru wa msingi wa kauli kwa kulazimisha kauli msizozipenda zinavunja amani. Wapi kumshawishi mtu ampigie kupiga kura mgombea wake kunavunja amani? Ikiwa mshawishika kakubali kusikiliza? Mbona we unamshawishi asisikilize?

    Mwachie uhuru wake wa kusikiliza na kuhukmu.

    ReplyDelete
  3. Shukran Mufti Mkuu kwa msimamo wa haki na usiopendelea upande wowote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...