Mshindi wa Tuzo ya Mama Shujaa mwaka 2011 inayotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kwa Mwanamke anaepambana na Ukatili wa Kijinsia Bi.Joyce Maimuna Amina Kanyamala ambae pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mikonoyetu la Jijini Mwanza akiwasilisha Mada katika Semina kwa Wanahabari kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa juu Vyombo vya Habari na Uchaguzi iliyoandaliwa na Chama cha cha Wanahabari Wanawake nchini Tanzania (TAMWA-Tanzania Media Women Association). 
Semina hiyo ilianza juzi Octoba 19 na inatarajiwa kufikia tamati hii leo Octoba 21 Jijini Mwanza.
Zaidi Mama Kanyamala aliwakumbusha wanahabari kuripoti na Kuandika habari za uchaguzi mkuu kwa ulinganifu sawa kwa kuzingatia Usawa wa Kijinsia.
Washiriki wa Semina hiyo (Wanahabari) waliahidi kutimiza majukumu yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuripoti habari za uchaguzi pamoja na nyinginezo nyingi kwa kuzingatia usawa baina ya wanaume na wanawake.
Mshindi wa Tuzo ya Mama Shujaa kwa Mwaka 2014 bi.Joyce Stephano akitoa ushuhuda wake kwa Wanahabari namna alivyopitia ukatili wa Kijinsia na namna alivyopambana nao na hatimae kuwasaidia wahanga wengine wa ukatili huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...