Bondia Thomas mashale wa manzese jijini Dar es salaam alifanya kitendo cha kusikitisha na kushangaza umma katika ukumbi wa friends corner uliopo Manzese ,pale alipomvamia katibu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Kamwe (bigright) kumpiga na kumpora simu na pesa. Akizungumza na vyanzo habari hizi Ibrahim kamwe alisema.”Nilikuwepo ukumbini hapo friends corner nikishuhudia mpambano wa Jonas Segu na idd Pearali kwa kuwa watu walikuwepo ni wengi mno na pale mbele kulikuwa na fujo za ushangiliaji nikaona ni bora nirudi nyuma kabisa ili nishuhudie kwa mbali , ghafla alitokea bondia huyo Thomas mashali akiwa na wenzake wanne akanishika mikono na wenzake kuanza kunisachi nilimputa mikono ili nizuie mifuko ndipo aliponipiga ngumi kali ya kidevuni na kichwani, watu walio karibu walipotugeukia sisi mashali na wenzake waliondoka haraka na kutokomea na simu yangu na kipochi akiniacha na maumivu ya kidevu.
Nilichokifanya ni kuripoti polisi na kupewa PF3 na RB ili
sheria ifuate mkondo wake.
Watu wengi waliokuwepo hapo ukumbini walisikitishwa na
vitendo vya bondia huyo kwa kuwa na
matukio kama hayo mfululizo bila kujali anaowafanyia ni kina nani kwani hivi
karibuni alimzuia kiongozi aliyekuwa akisafiri na bondia said mundi kuelekea
nchini Thailand kwa kumshikia chupa na wenzake wakiwa na visu na kuwapora simu
na pesa, bondia huyo wa tanga said mundi na Anthony ruta walikuwa wapole kwani
tukio hilo alilifanya muda mchache kabla ya kuelekea airport.
Thomas mashali ni mwingi wa matukio kama hayo hasa maeneo ya
manzese aliapa kujirekebisha kwa tabia hizo za ukabaji lakini inaonekana amerudi kivingine sasa hata
kwa watu anaowajua. Anafuatiliwa ili sheria ishike mkondo wakee
Duh! Huyo ni mwizi na sio bondia. Pole kwa wote waliopata madhara ya kichapo na kuibiwa. Ila asiachwe, sheria ifuate mkondo wake. Kama hawezi ngumu za mchezo arudi mtaani aendelee kukaba.
ReplyDeleteHuyu ni jambazi na anatumia ujuzi wake wa ngumi kwa njia ambayo siyo sahihi.
ReplyDeleteAchukuliwe hatua haraka na akafungwe ili aende akapambane na mabingwa wenzake huko jela.
Mambo gani haya jamani?
ReplyDelete