![]() |
MAREHEMU DKT. AMANDUS DAVID LWENA (Pichani)
KATIBU Mkuu Wizara ya
Kilimo Chakula na Ushirika anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi mwenzao
marehemu Dkt. Amandus David Lwena kilichotokea siku ya Ijumaa tarehe 02/10/2015
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Jijini, Dar es salaam.
Marehemu Amandus David Lwena alizaliwa tarehe 19/9/1962
katika hospitali ya Njombe. Mwaka 1973 - 1979 alimaaliza elimu yake ya msingi katika shule ya Msingi,
Kingole , Mkoani Mbeya.
Mwaka 1980-1983 alihitimu elimu ya sekondari, kidato
cha nne katika shule ya Sekondari ya Tosamaganga iliyopo Mkoani Iringa. Mwaka 1984 - 1986 alihitimu
elimu ya kidato cha sita katika shule ya sekondari Azania Mkoani Dar es salaam. Mwaka 1987-1991 alihitimu
Shahada ya Uhandisi wa Sayansi ya Kilimo katika chuo Kikuu cha kilimo Sokoine Sokoine
(SUA).
Marehemu Amandus David Lwena
alianza kazi mwaka 1991 katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (ARI) KATRIN mwaka 1994 aliamia Wizara ya Kilimo
Chakula na Ushirika katika Idara ya Umwagiliaji na Huduma za Ufundi ambapo
alifanya kazi katika nafasi mbalimbali mpaka umauti unamkuta, marehemu Amandus David Lwema alikuwa Mkurugenzi
Msaidizi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
Taifa limepoteza mtumishi
aliyekuwa mchapakazi na aliyefanya kazi kwa uweredi katika kipindi cha uhai
wake.
BWANA
AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE AMINA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...