Mkurugenzi
Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga amewahimiza waandishi wa habari
mkoani Dar es salaam kuzingatia maadili ya taaluma hiyo hasa wakati huu ambapo
taifa linaingia katika hatua muhimu ya kuchagua viongozi katika uchaguzi mkuu.
Mwamanga
ambaye alikuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa kongamano hilo amewasihi
waandishi wa habari kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya taaluma
yao ili kuepukana upotoshaji na kuitia nchi katika mgogoro usiokuwa wa lazima. Amesema
taaluma ya uandishi wa habari ina umuhimu mkubwa katika kujenga Jamii na
isipotumiwa vema inaweza kuhatarisha amani na utengamano wa taifa jambo ambalo
amesema halifai kufumbiwa macho.
Zifuatazo
ni baadhi ya picha za washiriki wa kongamano hilo lililofanyika kwenye ukumbi
wa hoteli ya PEACOCK mjini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji
wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga akifunga komgamano la waandishi wa habari wa
mkoa wa Dar es salaam lililojadili
utekelezaji wa uhuru wa habari kwa uangalifu hususani wakati huu wa kuelekea
kwenye uchaguzi mkuu.
Mkurugenzi Mtendaji
wa TASAF bwana Ladislaus Mwamanga (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na washiriki wa kongamano lililoandaliwa na chama cha waandishi wa
habari mkoa wa Dar es salaam baada ya kufunga rasmi kongamano hilo lililojadili
juu ya uchaguzi huru na haki bila waandishi wa habari kuzingatia maadili ni
ndoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...