Fundi Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Kenny Chitemo (aliyenyoosha mikono) akiwaonyesha Menejimenti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo moja ya mtambo wa masafa uliwekwa katika gari la masafa wakati menejimenti hiyo ilipofanya ziara katika ofisi za TCRA Jijini Dar es Salaam. Katikati mwenye koti la blue ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Sihaba Nkinga, na Kulia ni Mkurugenzi Mkuu TCRA Dkt. Ally Yahaya Simba.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga (wapili kulia) akiangalia mtambo wa masafa uliokua ukionyeshwa na Mhandisi Mwandamizi Masafa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw.Robson Shaaban (kulia) wakati Menejimenti ya Wizara hiyo ilipofanya ziara katika ofisi za TCRA Jijini Dar es Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu - Maelezo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...