Na Mwandishi Maalum, New York
Ikiwa ni Wiki moja kupita tangu Viongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka Mataifa mbalimbali Dunia, kuhitimisha ushiriki wao katika mikutano muhimu mikuu miwili, upitishwaji wa Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu na Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Nchi wanachama wameingia katika hatua nyingine ya mikutano ya Kamati Sita zinazounda Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Kamati zinazounda Baraza Kuu na ambazo zimeanza mikutano yake kuanzia Jumanne na itakayo kwenda hadi mwezi desemba kwa baadhi ya Kamati, ni Kamati ya Kwanza ambayo baadhi ya majukumu yake ni pamoja na udhibiti wa matumizi holela ya silaha za aina mbalimbali zikiwamo silaha za nyukilia , kemikali, silaha ndogo , kubwa na nyepesi , upokonyaji wa silaha na masuala yahusuyo ulinzi na usalama
Mikutano ya Kamati ya pili nayo imeanza, kamati ya pili inahusika na masuala yote ya uchumi, ikifuatia
Kamati ya Tatu inayohusika na masuala ya maendeleo ya Jamii, Utamaduni na Haki za Binadamu. Imeanza pia mikutano ya Kamati ya Nne inayohusika na masuala ya kumaliza ukoloni, operesheni za ulinzi wa Amani na masuala ya mawasiliano ya Umma,
Kamati nyingine ambazo zinaunda Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ni Kamati ya Tano ambayo inahusika na masuala ya Bajeti na Utawala ikifuatia na Kamati ya Sita inayohusika na masuala ya, pamoja na mambo mengine, sheria za kimataifa, utawala wa sheria na mahakama za kimataifa.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Uwakilishi wake wa Kudumu, inashiriki vema katika mikutano na mijadala yote ya Kamati hizi, ushiriki ambao pia unawahusisha wataalamu wa fani na kada mbalimbali kutoka Wizara na Idara za pande zote mbili za Muungano.
Akichangia majadiliano ya Kamati ya Tatu kuhusu ajenda ya Maendeleo ya Jamii,moja ya kati ya ajenda zitakazojadiliwa na Kamati hii, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi amesema, Tanzania imendelea na jukumu la kuhakikisha kwamba hakuna mtu wa rika lolote anayeachwa nyuma katika ajenda hiyo.
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi akichangia majadiliano kuhusu ajenda ya Maendeleo ya Jamii katika Mkutano wa Kamati ya Tatu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Kamati Sita zinazounda Baraza hilo zimeanza mikutano yake ikiwa ni wiki moja tangu kukamilika kwa mikutano ya Kilele ya Viongozi wa Kuu wa Nchi na Serikali iliyofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...