Ndugu  Issa BAtenga wa Dar es salaam anapenda kuchua nafasi hii kwa niamba ya familia kutoa tangazo kuwa Mwili wa Marehemu wa mama/shangazi/bibi yetu TAMALI LEBI MWAKYOMA.unawasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam alasiri ya leo Jumatano saa 9 kutoka India  na ndege ya Emirates. 

Utaratibu ni kwamba Mwili huo utapelekwa moja kwa moja kwenye Hospitali ya Aghakhan kwa ajili ya kuhifadhiwa na Maandalizi..
Taarifa hii ni kutokana na Kuvurugika kidogo kwa Ratiba za ujio wa watoto wa Marehemu waishio Marekani ambao utasababisha kukawia kwao kuwasili Tanzania, kwa kuzingatia haya na pia endapo watawasili siku ambazo hazitaendana na ratiba tulizozipanga hapo awali, ni dhahiri kwamba mwingiliano wa safari ya kwenda Mbeya-Tukuyu, mazishi na safari ya kurudi Dar es Salaam kabla ya Jumapili itakuwa imewakosesha waombolezaji na wafiwa haki zao za msingi za kupiga Kura siku ya Jumapili 25/10/2015. 


kwa hivyo na kwa kuzingatia haya, Tumeona ni busara tutoe tamko rasmi kwa kauli moja la kuahirisha Mazishi haya hadi tarehe ya karibu ambayo tutaipanga baada ya Uchaguzi.

Kwa ramani, Msiba upo barabara ya Rose Garden Mikocheni. kwa kutumia njia ya kutokea kwa Mwalimu Nyerere ni baada ya uzio wa TPDC/ Njia iendayo Data vision. Kuna kibao. 


Na kwa Barabara ya kutokea Maji Machafu/Sayansi, ni kwenye njia mita 100 kandokando ya je go la Tume ya Vyuo Vikuu (Commision of High learning Institutions) 
Tunawashukuru kwa uvumilivu na kwa kutufariji kila siku. 
Mungu Awabariki na awape nguvu wafiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...