2.0 Taarifa hii si ya ukweli na ni ya upotoshaji,Mhe Jaji Mkuu hajawahi kuzungumzia chochote kuhusu sheria hiyo ukitilia maanani kesi hiyo iko Mahakama Kuu shauri Namba 37 ya 2015 iliyofunguliwa na Bi. Amy Kibatala dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Uchaguzi (DE) na itatolewa maamuzi kati ya tarehe 22 au 23 mwezi huu. Hivyo, kwa mujibu wa sheria Mhe.Jaji Mkuu asingeweza kuzungumzia chochote kuhusu sheria hiyo kwa kuwa suala hilo liko MAHAKAMANI.                                                                                
  3.0 Tulimwandikia Mkurugenzi wa Habari MAELEZO nakala East Africa Television na kufuatilia kwenye Baraza la Habari (Media Council) kuomba maelezo ya kina na usahihi wa taarifa hiyo,  tarehe 21/10/2015 tumepokea barua Kumb Na EATV/ADMN/096/10/2015 ilyosaniwa na Bi Regina Mengi Mkurugenzi Mtendaji wa East Africa Television akiomba msamaha kuhusu taarifa hiyo potofu na kuwa watatoa maelezo ya ziada kuwa, taarifa hiyo haikutolewa na Mhe.Jaji Mkuu wa Tanzania
    Tunashukuru kwa ushirikiano mkubwa tulioupata toka uongozi wa juu kabisa wa East Africa Television kwa kuomba radhi mapema na Tunamini kuwa, vyombo vya Habari na Wananchi kwa ujumla vitasitisha usambazaji wa taarifa hii iliyokuwa si sahihi.
                                                                                                                                 Barua ya kuomba radhi imeambatanishwa:

 Imetolewa na:                     
MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA
                                              
MAHAKAMA                                                                   YA TANZANIA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tumesha zoea kulishwa uongo hata hilo hatuwezi kuliamini.kuna redio moja asubuhi kuna mtangazaji anajifanya shabiki wa chama fulani anasema mahakama tu ndoinaweza kutafsili.kusoma hajui nata kusikiliza hawezi.yaani uchaguzi huu umenipa elimu sana.nimejua mtanzania ni nani na yukoje.inasikitisha sana.

    Mungu atusaidie.elimu tulizopata zitusaidie.

    ReplyDelete
  2. Hii ni hatari kubwa hii TV siamini tena maishani mwangu na ni bora ifungiwe maisha ndugu zangu watanzania jirani zetu walianza na mambo kama haya matokeo yake MOTO uliowaka walishindwa kuuzima na kusababisha mauwaji ya kinyama mcheka na nyani huvuna mabuwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...