Afisa Mtendaji Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania Bw.Keith Tukei akikata utepe kuzindua duka la Vodacom la Ubungo lililopo eneo la flats za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wanaoshuhudia katikati ni Farida Yahya mteja wa kwanza kufika dukani hapo na  wa kwanza kulia ni Meneja wa duka hilo Bi.Jacqueline Twissa.
Baadhi ya wafanyakazi katika duka hili wakijiandaa kuanza kupokea wateja muda mfupi baada ya kuzinduliwa rasmi leo.
Wafanyakazi wa Vodashop Ubungo katika picha ya pamoja na maofisa wa Vodacom Tanzania muda mfupi baada ya kufunguliwa duka hilo leo.

KATIKA kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja iliyoanza leo jijini Dar es Salaam kampuni ya  mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua duka jipya la kisasa la kuhudumia wateja eneo la Ubungo kwenye nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa.

Akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa duka hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Keith Tukei amesema kuwa uzinduzi wa duka hili ni mwendelezo wa kampuni kusogeza huduma karibu kwa wateja.

“Vodacom kwetu wateja ni wafalme na siku zote tumekuwa tukisikiliza maoni yao na ndio maana tumeona kuna umuhimu wa kufungua duka eneo hili ili kuwarahishia wakazi wa ubungo kupata huduma zetu kwa urahisi bila kusumbuka kuzifuata mbali”.Alisema.

Aliongeza kuwa duka hilo mbali na kuuza simu za kila aina kwa gharama nafuu pia linatoa huduma mbalimbali kwa wateja ikiwemo huduma ya kutuma na kupokea fedha ya M-Pesa.

Kwa  upande wake Mkuu wa Kitengo cha huduma kwa wateja wa rejareja Brigita Stephen,alisema katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kampuni itakuwa na matukio mbalimbali ya kuwa karibu na wateja kwa kufungua maduka na  wafanyakazi wa Vodacom kusikiliza maoni ya wateja ili kuboresha huduma zaidi.

Aliwataka wateja wa Ubungo kutumia duka hili katika kupata huduma bora “Hili ni duka letu la 94 kufunguliwa nchini tunaendelea kusogeza huduma zetu na kuhakikisha zinawafikia wateja wetu kwa karibu na tuna imani wakazi wa Ubungo,Sinza,Mabibo,Manzese,Uzuri litawapunguzia usumbufu wa kufuata huduma zetu mbali”.Alisema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...