Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Ansgar Mushi.
Na Mwandishi wetu, Dodoma
WANACHAMA wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii wametakiwa kufuatilia makato yao kwa kuwa baadhi ya waajiri wanachelewa kupeleka makato yao.
Mbali na hilo, waajiri wa mmetakiwa kutowalazimisha wafanyakazi wao kujiunga na mfuko wasioupenda badala yake wapewe nafasi ya kujieleza.
Kauli hiyo, ilitolewa jana na Ofisa Tehama wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Kenneth Batanyita alipokuwa akitoa elimu kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi (TUCTA), mkoani Dodoma.
Mkurugenzi wa Utafiti, Tathmini na Sera kutoka SSRA,
Ansgar Mushi aliwatoa hofu wanachama wa mifuko hiyo, ya jamii kwa madai kuwa haiwezi kufa.
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi, Mkoa wa Dodoma,Ramadhani Mwendwa aliwataka wafanyakazi kujenga hoja wanapodai stahiki zao badala ya kulalamika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...