Baadhi ya wafanyakazi wa mfuko wa bima ya afya NHIF kigoma wakikabidhi msaada wa vyakula kwa uongozi wa kituo cha Silabu cha kulelea wazee wasiojiweza ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
Meneja wa Mfuko wa bima NHIF ya kigoma akisalimiana na wazee wanaotunzwa katika kambi ya Silabu kata ya kibirizi
Baadhi ya wazee wasiojiweza wanaoishi na kutunzwa katika
kambi ya kulea wazee ya Silabu kata ya Kibirizi Mkoani hapa
MFUKO wa Bima ya afya (NHIF)wametoa msaada wa vyakula kwa wazee wasiojiweza uliopo katika
kituo cha silabu kata ya kibirizi mjini hapa.
Akiongea baada ya kukabidhi msaada huo wa chakula Meneja wa
Mkoa wa mfuko huo Elius Odhiambo alisema kuwa mfuko unatumbua umuhimu na
mchango wa wazee kwa jamii.
"Sisi kama mfuko wa bima ya afya tuna thamini sana na
kutambua mchango wenu wazee kwa jamii kwani kila mmoja wetu ni mzee
mtarajiwa"alisema odhiambo
Alisema wamekabidhi msaada wa chakula wenye thamani ya
shilingi milioni moja na elfu sitini,vyakula walivyotoa ni mchele kilo
100,sukari kilo 100,unga wa ugali kilo 100,maharage kilo 100 na mafuta ya
kupikia kilo 20
Meneja huyo alisema wataendelea kusaidiana na kuwasaidia
wazee hao kila inapobidi.
Naye mkuu wa kituo hicho cha kutunzia wazee Juma Ndikamukana
wasiojiweza aliushukuru mfuko wa bima ya afya kwa msaada wao huo na kuwakumbuka
wazee katika siku yao leo.
Alisema kituo hicho kina jumla ya wazee 51 wasiojiweza
wanaotunzwa wanaotoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Kigoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...