KATIKA kuhakikisha wateja wake kutokuwa nyuma kiteknolojia na kupata huduma
bora za mawasiliano ya kisasa kwa kutumia mtandao wa intanet,kampuni
ya Vodacom Tanzania imezindua simu mpya ya Smart 6 ya gharama nafuu
ambayo wananchi wengi wanaweza kumudu kuinunua.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa simu hii Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni
hiyo,Kelvin Twissa amesema kuwa simu hii imelenga wateja
wake wenye vipato vya kawaida ili kuwawezesha kufurahia huduma za
kisasa za matumizi ya simu za mkononi za Smartphone ili waweze kwenenda
na teknolojia.
“Vodacom
siku zote tumekuwa tukiwasikiliza wateja wetu na ndio maana tumeingiza
sokoni simu hii ili kuwawezesha kufurahia matumizi ya
simu za kisasa za smart ambazo zinawawezesha kupata huduma za internet
na program nyinginezo za kurahisisha maisha yao na kuwa murua ikiwemo
kupiga picha wazipendazo kwa kutumia simu zao,”Alisema Twissa.
Aliongeza
kuwa simu hii ya Smart 6 ambayo itakuwa inauzwa kwa bei nafuu kabisa ya
shilingi 90,000/- ina kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji
kusoma na kuangalia taarifa kwa urahisi,ina kamera ya kisasa,uwezo
zaidi wa kuperuzi intanet ya 3G, nafasi kubwa ya kuweka kumbukumbu na
inakaa na betri kwa muda mrefu. Hii ni simu ya kipekee ambayo kila mteja
anatakiwa kuwa nayo.
Alisema
simu hizi zinapatikana katika maduka yote ya Vodacom na katika
matamasha yote yanayofanywa na kampuni yetu nchi nzima ya Vodacom
tumekufikia.Mteja yeyote atakayenunua simu hii atajipatia ofa kabambe
kabisa ya kupata 500MB bure na uwezo wa kutuma jumbe fupi za maneno
zipatazo 200 kila mwezi kwa kipindi cha miezi 6 bure.
Aliwataka
wateja wa Vodacom na wananchi wengine kwa ujumla kuchangamkia fursa hii
na kukamata Smart 6 kwa gharama nafuu ili kuendelea kupata
taarifa za huduma mbalimbali zinazopatikana kwa kuperuzi mtandao wa
intanet.Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu
www.vodacom.co.tz au kurasa zetu za Facebook
na Twitter.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(kushoto)akiwanesha waandishi wa habari(hawapo pichani) simu mpya aina ya Smart 6 wakati wa uzinduzi wa simu hiyo yenye kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji kusoma na kuangalia taarifa kwa urahisi na ina kamera ya kisasa na uwezo zaidi wa kuperuzi intanet ya 3G,itapatikana kwa bei nafuu kabisa shilingi 90,000/- inapatikana katika maduka yote ya kampuni hiyo.Mteja yeyote atakayenunua simu hiyo atajipatia ofa kabambe kabisa ya kupata 500MB bure na uwezo wa kutuma jumbe fupi za maneno zipatazo 200 kila mwezi kwa kipindi cha miezi 6 bure.Kulia ni Mkuu wa huduma na bidhaa wa kampuni hiyo,Samson Mwongela.
Mkuu wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Mwongela(kulia)akimshuhudia Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(kushoto)akiwanesha waandishi wa habari(hawapo pichani) simu mpya aina ya Smart 6 wakati wa uzinduzi wa simu hiyo yenye kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji kusoma na kuangalia taarifa kwa urahisi na yenye kamera ya kisasa na uwezo zaidi wa kuperuzi intanet ya 3G, itapatikana kwa bei nafuu kabisa shilingi 90,000/- inapatikana katika maduka yote ya kampuni hiyo.Mteja yeyote atakayenunua simu hiyo atajipatia ofa kabambe kabisa ya kupata 500MB bure na uwezo wa kutuma jumbe fupi za maneno zipatazo 200 kila mwezi kwa kipindi cha miezi 6 bure.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom
Tanzania,Kelvin Twissa(kushoto) pamoja na Mkuu
wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Mwongela,wakijipiga
selfiii kwa kutumia simu mpya aina ya Smart 6 waliyoizindua leo
yenye kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji kusoma na kuangalia
taarifa kwa urahisi na yenye kamera ya kisasa na uwezo zaidi wa kuperuzi
intanet ya 3G,
itapatikana kwa bei nafuu
kabisa shilingi 90,000/- katika maduka yote ya kampuni hiyo.Mteja
yeyote atakayenunua simu hiyo atajipatia ofa kabambe kabisa ya kupata
500MB bure na uwezo wa kutuma jumbe fupi za maneno zipatazo 200 kila
mwezi kwa kipindi cha miezi 6 bure.
Vodacom launches the affordable Smart 6 phone
In ensuring that their customers stay connected to the latest technology, and that they get the best services and communications using Internet, Vodacom Tanzania has introduced yet another smartphone; the Smart 6 which is the most affordale smartphone .
Speaking during the launch, Vodacom Tanzania’s Head of Marketing and Communication,Kelvin Twissa said the phone price is Tshs 90,000 and will enable many customers to enjoy the modern amenities of the Smart phone and keep up with technology.
“The Smart 6 is the latest Vodacom device to launch in Tanzania with the express purpose of making the cost to connect more affordable,” said Twissa.
The Smart 6 comes with the latest Android application, features a 4-inch WVGA display for better viewing experience, 4GB internal storage, 1GHz dual-core processor and can support internet speeds of upto 21mbps.With a Longer Battery Life and at a price that most citizens can afford, this is everyones smartphone.
Additionaly, customers get 500MB and 200 free text messages for a period of 6 months. The device will be available in our Vodacom shops and authorized dealers and promoters countrywide.
For more details visit our website www.vodacom.co.tz or follow us on Facebook/Twitter .
Usiniminyie mtundiko wangu:
ReplyDeleteHivi hizi simu, tusizotengeza, zinabadilika kila baada ya miezi mingapi ili wapate faida watengenezaji?
Sio lazima kununua kila sampli mpya inayoingia; ni mrija wa kufonza (vacuum) utajiri wa Watanzania masikini, ama sivyo?