Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
IKIWA  zimebakia siku nane kufikia Uchaguzi Mkuu, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda  amewataka wananchi wa wilaya hiyo kusimamia amani na utulivu wa nchi  bila kufanya hivyo  ahadi za wagombea wote hazitoweza kutekelezeka na badala yake kuanza kuugua maumivu ya uchaguzi huo

Makonda ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni pamoja na wenyeviti  wa serikali za mitaa, wagombea wa ngazi mbalimbali za uongozi, wasimamizi wa uchaguzi na viongozi wa vyama vya siasa .

“ Sisi sote tunatoka katika itikadi tofauti tofauti lakini wote tupiganie maendeleo yaTaifa kwa ujumla kuweza kupiga kura kwa staha kuweza kulinda amani na vikundi vyovyote visiweze kukaa katika eneo la kupigi kura" amesema Makonda.

Amesema Wilaya ya Kinondoni isiwe chanzo cha kusambaza chuki na kwamba kila mwenyekiti wa serikali ya mtaa ajitambue kuwa ana mamlaka tosha yakusimamia na kutekeleza uwepo wa amani.

Makonda amesema viongozi wa mitaa wao ndio wenye mamlaka tosha ya kuhakikisha maeneo wanaoishi yanabakia kuwa na amani wakati wa upigaji kura na wakati wa kusubiria matokeo.

Amesema yapo baadhi ya maeneo ambayo watumishi wa serikali wanashindwa kutekeleza wajibu wao ili kuibua chuki kwa wananchi kuwa serikali haiwajibiki kwao, hivyo viongozi wa mitaa watakapooona hali kama hizo wawajibuike kutoa taarifa.

Aidha  Makonda amepiga marufuku  vikundi vinavyoundwa  kwa ajili ya kusimamia kura na kwamba pindi akipata taarifa atawashughulika nao bila aibu katika kuweza  kumalizika kwa uchaguzi huku amani ikitawala.

Nae Mkurugenzi wa Kinondoni, Mussa Natty amesema suala la ulinzi na usalama  ni la kila mtu  na  kuwataka viongozi wa mitaa kutoa taarifa ya kile kinachofanyika katika maeneo yao.


Amesema wananchi wanatakiwa kukaa mita 200 baada ya kupiga kura, na kama kuna kijiwe ambacho kina wakereketwa wasiwepo  katika eneo hilo ni amri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Serikali isisitize kuwa watu wafuate sheria. Serikali yenyewe ifuate sheria. Sheria ya uchaguzi inaruhusu watu wakishapiga kura kuwepo nje ya mita 200 kutoka kituoni. Nje ya hizo mita 200, watu wana haki na uhuru kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa amani. Wa-Tanzania wanapenda kukaa vijiweni. Wakianzisha vijiwe nje ya hilo eneo linalotajwa katika sheria, wana haki na uhuru wa kufanya hivyo. Haijalishi kama vijiwe hivi ni vya kawaida vya kupigia gumzo au kulinda kura kama wanavyoamini wengi wao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...