Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
IKIWA zimebakia siku nane kufikia Uchaguzi Mkuu,
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amewataka wananchi wa wilaya hiyo kusimamia
amani na utulivu wa nchi bila kufanya hivyo ahadi za
wagombea wote hazitoweza kutekelezeka na badala yake kuanza kuugua maumivu ya uchaguzi huo
Makonda ameyasema
hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni pamoja na wenyeviti
wa serikali za mitaa, wagombea wa ngazi mbalimbali za uongozi,
wasimamizi wa uchaguzi na viongozi wa vyama vya siasa .
“
Sisi sote tunatoka
katika itikadi tofauti tofauti lakini wote tupiganie maendeleo yaTaifa
kwa ujumla kuweza kupiga kura kwa staha kuweza kulinda amani na vikundi
vyovyote visiweze kukaa katika eneo la kupigi kura" amesema Makonda.
Amesema Wilaya ya Kinondoni isiwe chanzo cha kusambaza chuki na kwamba kila mwenyekiti
wa serikali ya mtaa ajitambue kuwa ana mamlaka tosha yakusimamia na kutekeleza
uwepo wa amani.
Makonda
amesema
viongozi wa mitaa wao ndio wenye mamlaka tosha ya kuhakikisha maeneo
wanaoishi yanabakia kuwa na amani wakati wa upigaji kura na wakati wa
kusubiria matokeo.
Amesema yapo
baadhi ya maeneo ambayo watumishi wa serikali wanashindwa kutekeleza wajibu wao
ili kuibua chuki kwa wananchi kuwa serikali haiwajibiki kwao, hivyo viongozi wa
mitaa watakapooona hali kama hizo wawajibuike kutoa taarifa.
Aidha
Makonda amepiga marufuku vikundi vinavyoundwa kwa ajili ya kusimamia kura na kwamba pindi
akipata taarifa atawashughulika nao bila aibu katika kuweza kumalizika kwa uchaguzi huku amani ikitawala.
Nae Mkurugenzi wa Kinondoni, Mussa Natty amesema suala la ulinzi na
usalama ni la kila mtu na kuwataka viongozi wa mitaa kutoa taarifa ya kile kinachofanyika katika maeneo yao.
Amesema
wananchi wanatakiwa kukaa mita 200 baada ya kupiga kura, na kama kuna kijiwe
ambacho kina wakereketwa wasiwepo katika
eneo hilo ni amri.
Serikali isisitize kuwa watu wafuate sheria. Serikali yenyewe ifuate sheria. Sheria ya uchaguzi inaruhusu watu wakishapiga kura kuwepo nje ya mita 200 kutoka kituoni. Nje ya hizo mita 200, watu wana haki na uhuru kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa amani. Wa-Tanzania wanapenda kukaa vijiweni. Wakianzisha vijiwe nje ya hilo eneo linalotajwa katika sheria, wana haki na uhuru wa kufanya hivyo. Haijalishi kama vijiwe hivi ni vya kawaida vya kupigia gumzo au kulinda kura kama wanavyoamini wengi wao.
ReplyDelete