Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya utofauti wa itikadi wa vyama ndiyo ukomavu wa demokrasia nchini hivyo ni jambo la busara kuvumiliana na kufanya siasa za kistaarabu, ameyasema hayo wakati wa kikao hicho kimefanyika leo jijini Dar es Salaam kulia ni Balozi wa Amani Mrisho Mpoto na kushoto ni Balozi wa Amani Christina Shusho.
Balozi wa Amani Mrisho Mpoto akifafanua jambo katika kikao hicho leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka)
Na Magreth Kinabo-maelezo
OFISIya Msajili wa Vyama Vya Siasa imewaasa na kuwataka viongozi wote wa vyama vya siasa kutoa kauli na maelekezo kwa wafuasi wao na wanachama wa vyama vyao kutoshiriki katika aina yoyote ile ya uvunjifu wa amani hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo.
Hayo yamesemwa leo na Msajili wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis Mutungi wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi hiyo jijini Dares Salaam.
“Dhamana ya nchi iko mikononi mwenu,ushawishi wenu kuhusu amani katika kipindi hiki ndio utakaoliokoa taifa la Tanzania ama utaliingiza taifa katika vurugu na mfarakano,” alisema Jaji Mutungi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...