Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi
CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia umati wa watu kweny mkutano wa
kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa shule ya msingi Mpili pili mkoani Lindi,
Katika
mkutano huo wa hadhara Dkt.John Pombe Magufuli amesema kuwa Serikali
atakayounda baada ya kuchaguliwa na Watanzania Oktoba 25 mwaka huu,
itahakikisha inawatumikia huku akiweka wazi kuwa yeye hakuwa na mchezo kwani dhamira yake ni kutatua shida za wananchi kwa spidi kubwa.
Amesema
anatambua shida ambazo watanzania zinawakabili na hivyo uamuzi wake wa
kuomba nafasi hiyo ni kuhakikisha anakabiliana nazo huku akisisitiza
serikali yake,Mawaziri atakaoteua wajiandae kufanya kazi na atakayeona
hawezi ni bora akajiweka pembeni mapema kabla ya kuapishwa ama akakataa
uteuzi.
Dkt Magufuli pia ametumia nafasi hiyo kuwapongeza Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya wali0jinyakulia
tuzo hizo usiku wa kuamkia leo huko Dallas, Marekani ambapo Diamond
alichukua tuzo tatu katika vipengele vya Best Dance Video kupitia wimbo
wake wa Nana, Best Male East Africa Artist na Artist of The Year huku
wimbo wa Alive alioshirikiana na Brackets ukichukua tuzo ya Best
Inspirational Song of The Year.
Wakati
huohuo mwanadada, Vanessa Mdee akichukua tuzo ya Best Female East
Africa huku Ommy Dimpoz akichukua tuzo ya Best New Comer na kufanya
Tanzania kukusanya jumla ya tuzo tano.
Dkt Magufuli amefanya kampeni zake katika jimbo la Nachingwea,Ruangwa,jimbo la Mtama na Lindi mjini huku akisimamishwa na wanachi mara kadhaa kila alikokuwa anapita.
Dkt Magufuli amefanya kampeni zake katika jimbo la Nachingwea,Ruangwa,jimbo la Mtama na Lindi mjini huku akisimamishwa na wanachi mara kadhaa kila alikokuwa anapita.
Sehemu
ya umati wa kazi wa mji wa Lindi Mjini wakishangilia wakati Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake za kuomba kura ya
kuwania nafasi ya Urais.
Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM,Mama Salma Kikwete akimuombea kura za kutosha
mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni
uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Mpili pili mkoani Lindi
jioni ya leo.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia mkutano wa kampeni a Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli mjini Lindi.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli akimuombea kura kwa wananchi Mgombea Ubunge
wa jimbo la Mtama,Ndugu Nape Nnauye kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli.
Mjumbea
wa kamati ya ushindi ya kampeni za Mgombea Urais wa CCM,Mh Bernad Membe
akiwahutubia wananchi wa Lindi mjini kwenye mkutano wa kampeni wa
Mgombea Urais wa CCM zilizofanyika katika uwanja wa shule ya msingi
mpili pili,mkoani Lindi.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi
mgombea Ubunge wa jimbo la Ruangwa,Mh.Kassim Majaliwa,kwenye mkutano wa
kampeni uliofanyika leo mchana mjini Ruangwa mkoani Lindi mara bada ya
kumkabidhi kitabu cha Ilani ya CCM.
Mmoja
wa wafuasi wa chama cha CHADEMA akizungumza mbele ya umati mkubwa wa
wakazi wa mji wa Ruangwa mara baada ya kurejesha kadi ya chama chake kwa
Mgombea Urasi wa CCM Dkt Magufuli,ambapo wanachama wapatao 150 wa vyama
mbalimbali pinzani walirejsha kadi zao.
Wananchi
wa jimbo la Mtama wakishangilia jambo wakato mgombea Urais wa CCM Dkt
John Pombe Magufuli alipokuwa akizimwaga sera zake za kuomba nafasi ya
kuwania Urais wa awamu ya tano ifikapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa
mwaka huu utakaohusisha nafasi ya Urais,Wabunge na Madiwani.
CCM tuko tayari awamu ya tano ni kazi tu.
ReplyDelete