Harakati
za kusaka nafasi ya juu ya uongozi katika
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo zimepiga kambi mkoani
Singida kwa mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt John Pombe
Magufuli pichani kuwahutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika
uwanja wa Peoples mjini humo kwenye mkutano wa kampeni.
Dkt
Magufuli ameishauri tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kutimiza wajibu wake
wa kutenda haki kwa wagombea wote wa ngazi za Uraisi,pia amewataka
Wananchi wakatae kulaghaiwa na baadhi ya watu wanaotaka madaraka kwa
nguvu,kwa kuzinunua shahada zao za kupigia kura,badala yake amewaomba
wazitunze shahada hizo ili ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wapige kura.
Maelfu
ya Wananchi wa Singida wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli
alipokuwa akiwahutubia na kujinadi kwa kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza
iwapo watamchagua kuwa Rais ifikapo Oktoba 25 mwaka huu,kwenye uchaguzi
mkuu,Dkt Magufuli amewaomba wananchi hao alipokuwa akiwahutubia kwenye
mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Peoples ,mjini Singida.
Wakazi wa mji wa Singiga na vitongoji vyake wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuwaomba wampigie kura za ndio ifikapo Oktoba 25 Mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu wa Urais,Wabunge na Madiwani.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi,Dkt Joh Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la
Singida mjini Mussa Sima mbele ya maelfu ya Wananchi (hawapo pichani)
kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Peoples mjini Singida jioni ya leo.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Iramba Magharibi kwa wakazi wa Iramba mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,mara baada ya kumkabidhi Ilani ya chama hicho.
Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukikatiza katika bonde la Sibiti kupitia barabara ya Nduguti kuelekea wilayani Mkalama,kwenye mkutano wa kampeni mapema leo mchana.
Ujenzi wa Daraja la Sibiti wilayani Mkalama likiwa katika hatua za mwisho kukamilika,Daraja hilo limeleta matumaini mapya kwa wakazi hao wa Mkalama,kwani wakati wa mvua ilikuwa ni kikwazo kikubwa kwao wakati wa kusafiri na hata kusafirisha mazao yao ya biashara.
Wananchi wa Singida na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa People's,mjini Singida katika mkutano wa kampeni wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kabla ya kuanza kuwahutubia jioni ya leo.
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akiwaomba wakazi wa mji wa Singida na vitogoji vyake waliofurika kwenye mkutano wa kampeni,kuwa ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wajitokeza kwa wingi kumpigia kura za ndio za kutosha Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na Mbunge na Madiwani ili wapate ushindi wa kishindo.
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni CCM,Ndugu January Makamba akimuombea kura za kutosha mmgomea Urais wa CCM Dkt Maguli pamoja na Mbunge na Madiwani wa Singida mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Peoples mjini humo.
Baadhi ya Kadi za Wanachama wa Chadema zilizokabidhiwa kwa Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Kiomboi,Wilayani Iramba mapema leo mchana.
Maelfu ya wakazi wa Singida wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,uliofanyika katika uwanja wa Peoples mjini humo.
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mjini (Mbunge Mstaafu),Mohamed Dewji akimwombea kura Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa Singida na vitongoji vyake katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Peoples ,mjini Singida,Dewji pia ametangaza kumuunga mkono aliyemrithi kiti chake cha Ubunge,Ndugu Mussa Sima.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...