Waziri wa  Nchi  Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Mh. Dk. Binilith Mahenge (wa kwanza kushoto), akijadiliana  na Balozi wa Uswisi  nchini, Bi Florence Tinguely Mattli (katikati),  kuhusu Mkataba wa Mazingira wa Minamata unaohusu matumizi ya Kemikali ya Zebaki na Madhara yake katika Mazingira, Majadilaino hayo yamefanyika katika Ofisi ya Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na  Katibu Mkuu wa Ofis hiyo Bw. Sazi Salula (kulia), jijini Dar es Salaam leo
 Waziri wa Nchi Ofis ya Makamu wa Rais Mazingira Mh. Binilith Mahenge akiwa kwenye picha ya pamoja na Baloz wa Ufaransa nchini, pamoja na wageni waliotembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam  kwa ajili  kujadili  mchango wa Tanzania katika Mkutano wa Ishirini na Moja wa nchi wanachama wa Mkataba Mpya wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika jijini Paris nchini Ufaransa Desemba mwaka huu.
Waziri wa Nchi  Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mh. Dk. Binilith Mahenge akiwa na Balozi wa Ufaransa nchini, Bi  Malika Berak wakionesha nyaraka zinazungumzia mchango wa Tanzania katika Mkataba mpya wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika katika Mkutano wa Ishirini na Moja wa nchi wanachama wa Mkataba huo jijini Paris, Ufaransa Desemba mwaka huu. Picha na OMR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...