
Dk. Bhuvaneshwari Shankar, Mkuu wa idara ya lishe kutoka hospitali za Apollo.
Na Mwandishi Wetu,
Novemba
14 kila mwaka tunaadhimisha siku ya kisukari duniani ili kuongeza
uelewa kuhusu madhara ya kisukari, matatizo yanayoletwa na huu ugonjwa
na taarifa muhimu kuhusu kisukari.
Siku
hii inabeba ujumbe mahususi kwa watu wote ulimwenguni. Kauli mbiu
katika siku hii tokea 2014 hadi 2016 ni maisha bora na kisukari(healthy
living and diabetes) na mwaka huu kuna mtazamo zaidi katika kuzingatia
mlo kamili na kuanza kila siku na kifungua kinywa bora.
Kutoka
katika shirika la kisukari Africa, Tanzania ni kati ya nchi 32 katika
shirikisho hilo kwa viwango vya nchi zenye viwango vya kisukari duniani.
Kulikuwepo na zaidi ya kesi milioni 1.7 za kisukari hapa Tanzania kwa
mwaka 2014. Shirika la afya duniani (WHO) linakadiria zaidi ya watu
milioni 180 ulimwenguni wana kisukari, na hiyo takwimu inatarajiwa
kuongezeka ifikapo mwaka 2030 kama hamna hatua yoyote itakayochukuliwa.
SOMA ZAIDI HAPA
SOMA ZAIDI HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...