Mwenyekiti
na Mkurugenzi Mtendaji wa Motisun Group Subhash Patel (wapili kushoto)
akiwasha mshumaa pamoja na wawakilishi wa makampuni tanzu za Motisun
Group kuashiria uzinduzi wa mabati ya Kiboko Imara. Hafla ya uzinduzi
ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar-es-salaam.
Balozi
wa mabati ya Kiboko Jacob Steven ‘JB’ akicheza ngoma ya asili na
kikundi cha KP traditional dance katika uzinduzi wa mabati ya Kiboko
Imara yanayotengenezwa na kampuni ya MMI STEEL. Hafla ya uzinduzi
ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar-es-salaam.
Mwenyekiti
na mkurugenzi mtendaji wa Motisun Group Subhash Patel akimvalisha taji
balozi wa mabati ya Kiboko Imara Jacob Steven ‘JB’ katika uzinduzi wa
mabati ya Kiboko yanayotengenezwa na kampuni ya MMI STEEL. Hafla ya
uzinduzi ulifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar-es-salaam.
Kampuni
inayozalisha vifaa vya ujenzi, iitwayo Motisun imezindua teknolojia
itakayoongeza ubora na kuimarisha vifaa kama mabati kwa ajili ya
kuezekea paa za nyumba na majengo.
Teknolijia
hiyo ilizinduliwa jijini Dar es Salaam katika Hotel ya Sea Cliff na
kutangazwa kuanza kwa shughuli ya uuzaji wa mabati hayo katika maeneo
mbalimbali nchini na nje ya nchi.
Mwenyekiti
na Muasisi wa kampuni ya Motisun, Subhash Patel alisema, teknolojia hii
inahusu utumiaji wa madini ya aluminiamu na zinki ambayo huongeza ubora
na kuyafanya mabati kudumu zaidi.Alisema
bidhaa hii mpya itakuwa ikipatikana chini ya kampuni tanzu ya Motisun
iitwayo MMI. Bidhaa zitakuwa zikiuzwa katika maduka ya rejareja hususani
katika maeneo ambapo wateja hupendelea bidhaa za ubora wa hali ya juu.
“Bidhaa
hii itakuwa inajulikana sokoni kwa jina la Kiboko Imara. Ili
kuiunganisha na walaji, Kiboko Imara itakuwa ikitangazwa na Msanii
maarufu Jakobo Stephen ambaye anafanya zivuri katika fani yake na kuwa
na mvuto kwa wengi,” alisema.
Bwana
Patel anasema kuzinduliwa kwa bidhaa mpya kunaashiria juhudi za kampuni
ya MMI kuongeza wigo wa bidhaa kwa kuzingatia mahitaji ya teknolojia
ambayo ina manufaa mengi katika sekta ya ujenzi.
Kampuni
ya MMI ni maarufu kwa uzalishaji wa bidhaa za ujenzi kama nondo ambazo
zimekuwa zikiuzwa ndani na hata nchi jirani za Msumbiji, Zambia na
Uganda zikiambatana na ubora.
“Tumejiandaa
kikamilifu kuifanyia mauzo bidhaa hii mpya katika masoko hapa nchini na
nchi jirani ambapo pia kuna fursa ya masoko,” alisema bwana Patel.Bidhaa
za mabati zilizopakwa madini ya aluminiam na zinki zimekuwa
zikikubalika sana katika masoko mengi duniani kwa ajili ya makazi ya
kuishi na majumba makubwa ya biashara ambayo huweka msisitizo katika
viwango vya ujenzi.
Alisema
tayari kuna wimbi kubwa la asili la watu kuhamia katika matumizi ya
mabati yaliyopakwa madini ya aluminiamu na zinki kutokana na kuwa na
uwezo wa kudumu kwa muda mrefu.
“Ni
kwa sababu hii MMI imechagua kuzalisha bidhaa hii muhimu nchini
Tanzania kwa matumizi ya makazi ama miradi ya biashara,” alisema bwana
Patel.
Bidhaa hii ya Kiboko Imara inatoa wigo mpana kwa matumizi mbalimbali mfano urefu, rangi na hata unene wa mabati. “Hii
inamaanisha mapaa mbalimbali huhitaji unene na urefu tofauti wa mabati,
mfano nyumba ya kuishi inahitaji mabati yenye unene wa kawaida wakati
paa za majengo ya viwanda na biadhara kubwa kubwa huhitaji mabati manene
zaidi,” alisema.Kwa
mujibu wa bwana Patel, utengenezaji wa bidhaa hii mpya umezingatia
viwango vya kitaifa na kimataifa kwani zimejaribiwa ili kukidhi viwango
vya ubora.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...