
Meneja mauzo Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel, Aluta Kweka ( kulia) pamoja na Mkuu wa wilaya ya
Korogwe,Hafsa Mtasiwa (wa kwanza kushoto) akifatia na Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Patricia Andrew Mbigili
(katikati) wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya
mazinde Day wakionyesha vitabu walivyokabidhi na Airtel ikiwa na lengo
la kutatua changamoto ya uhaba wa vitabu shuleni hapo. Vitabu hivyo
vya sayansi vinathamani ya shilingi milioni 3.
KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa Airtel
shule yetu imetoa msaada wa vitabu vyenye thamani ya sh.milioni tatu
kwa Shule ya Sekondari ya mazinde Day ya mkoani wa Tanga wilaya ya
Korogwe.
Akikabidhi msaada huo jana Meneja mauzo Kanda ya Kaskazini Aluta Kweka
alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kuendeleza elimu nchini Airtel
ililazimika kuanzisha mpango huo ili kuongeza viwango vya ufaulu.
Alisema kuwa vitabu vilivyotolewa ni vya sayansi hivyo kupitia vitabu
hivyo wanafunzi wataongeza bidii kwa kuvisoma na kusaidia idadi ya
wanafunzi wanaofaulu katika masomo hayo ambayo awali ilionekana ni
masomo magumu kutokana na kutokuwa na vitendeakazi.
Alisema kuwa utoaji wa vitabu hivyo kwa shule za sekondari ni mmrefu
unaofanywa na kampuni yake ili kutimiza dhamira yake ya kurudisha
faida wanayopata kwa Watanzania na kuboresha huduma mbalimbali za
kijamii.

Meneja mauzo Kanda ya Kaskazini wa Airtel, Aluta Kweka akimkabidhi
vitabu vya sayansi mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mazinde Day,
Bi Jermana Mchome (katikati) ikiwa ni msaada katika kuendeleza elimu
na kutatua changamoto za uhaba wa vitabu shuleni hapo. Akishuhudia ni
Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Hafsa Mtasiwa.
Alisema kuwa hadi sasa zaidi ya shule 1,300 zimenufaika na mradi huo
ambapo umechangia kupunguza changamoto ya ukosefu wa vitabu kwa shule
zilizokabidhiwa.
Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo Mkuu wa wilaya ya Korogwe
Hafsa Mtasi aliipongeza kampuni hiyo ambapo imekuwa ikisaidiana na
serikali katika kuinua kiwango cha elimu nchini.
"Tunaipongeza Airtel kwa mpango huu kwani umekuwa ukichangia kupunguza
changamoto ya ukosefu wa vitabu katika shule za sekondari na ni mfano
mzuri wa kuigwa," alisema.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Mazinde Day,Jermana Mchome
aliishukuru Airtel pamoja na kuwasisitiza wanafunzi wa shule zote
zilizofaidika kuvitumia vitabu kikamilifu ili kujiendeleza kwa manufaa
ya jamii zao pamoja na taifa kwa ujumla.
"Sasa ni jukumu lenu wanafunzi kutumia fursa hii kusoma kwa bidii ili
muweze kusaidia taifa baada ya kisomo chenu, msaada huu mkiutumia
vizuri ni nyenzo kubwa sana yakusaidia hata familia zenu kutokana na
faida kubwa mtakayopata kutokana na zao la elimu” alisema.
Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia
sekta ya elimu kupitia mpango wake wa Airtel Shule Yetu bado inasaidia
vijana mbalimbali hapa nchini kutatua changamoto mbalimbali kupitia
mradi wake mpya wa Airtel FURSA Tunakuwezesha

Meneja mauzo Kanda ya Kaskazini wa Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel, Aluta Kweka (kushoto) pamoja na Mkuu wa wilaya ya Korogwe
,Hafsa Mtasiwa na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Mazinde Day,
Jermana Mchome (katikati) wakionyesha vitabu walivyokabithi na Airtel
ikiwa na lengo la kutatua changamoto ya vitabu shuleni hapo. Vitabu
hivyo vya sayansi vinathamani ya shilingi milioni 3.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...