Wawezeshaji wa Sheria katika soko la Mchikichini katika Manispaa ya Ilala, wakiwa na mabango ya mradi wa Mpe Riziki si Matusi baada ya kuzungumza na waaandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wanaotembelea masoko yaliyopo katika Manispaa hiyo kuona maendeleo ya vita ya  kupinga udhalilishaji wa kijinsia katika masoko hayo baada ya Shirika la Equality for Growth linaloendesha mradi huo kutoa mafunzo kwa Wawezeshaji wa Sheria wanaoshirikiana na wafanyabiashara katika vita hivyo.
Mwezeshaji wa Sheria, Eva Kakobe akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya ukatili wa jinsia wanavyokabiliana nayo katika soko hilo.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Na Dotto Mwaibale
VYUMBA vilivyokuwa vikitumiwa kwa ajili ya kupimia nguo kabla ya kuzinunua katika soko la Mchikichini Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam vinadaiwa vilikuwa vikitumia kudhalilidha wateja hasa wanawake.

Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Bodi ya Sekta ya Kanga na Vitenge katika soko hilo Zainabu Namijojo Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akizungumza na waandishi wa habari ambao wanafanya ziara ya kutembea masoko ya Manispaa ya Ilala kuona jinsi mradi wa Mpe Riziki si Matusi ulivyowakomboa wanawake katika vita ya kupinga udhalilishaji masokoni unaoendeshwa na Shirika la Equality for Growth (EfG).

"Katika soko letu tulikuwa na changamoto kubwa ya udhalilishaji hasa maeneo ya wauza nguo kuu kuu (Mitumba), kwani walikuwa wakitumia vyumba vidogo vya kujaribishia nguo kuwadhalilisha wanawake kwa kuwakamata maungoni na kuwawekea kioo chini ili waweze kuona utupu wao" alisema Namijojo.

Alisema hivi sasa vitendo hivyo vimekoma baada ya shirika hilo kufanya matamasha na semina mbalimbali na kutoa mafunzo kwa baadhi yao ambao sasa ni Wawezeshaji wa Sheria katika soko hilo ambao wamekuwa karibu na wafanyabiashara kufuatilia vitendo vya udhalilishaji.

Mwezeshaji wa Sheria Domitila Ngwada alisema vitendo vya ubakaji na matusi ya nguono yalishamiri sana lakini hivi sasa hali ni nzuri kwani vitendo hivyo vimepungua kwa asilimia 70 ukilisha na hapo awali kabla ya kufikiwa na EfG.

"Tangu kuwepo na wawezeshaji wa Sheria katika soko letu vijana wengi waliokuwa na vitendo vya kudhalilisha wanawake wameingiwa na hofu kubwa hasa kupigwa faini zilizowekwa kuanzia kiwango cha sh.50,000" alisema Ngwada.

Mfanyabiashara katika soko hilo, Ikram Zuberi alisema jitihada za makusudi zinapaswa kufanyika ili kumaliza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika sokjo hilo ingawa kwa kiasi kikubwa vimepungua kwa msaa wa EfG.

Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo Charles Beatus alisema wale wote wanaopatika na makosa ya udhalilishaji wamekuwa wakiadhibiwa kutokana na mwongozo uliopo na kesi zote zinaanza kusikilizwa sokoni hapo na ikishindikana upelekwa ngazi nyingine ikiwemo polisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...