Katika juhudu zake za kuhakikisha watanzania waishio mjini na vijiji
wanapata huduma bora za mawasiliano , kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
leo imezindua mnara wa mawasiliano katika kata ya mazinde wilaya ya
Korogwe, mkoani Tanga.
Uzinduzi huo wa mnara wa mawasiliano utawahakikishia wakazi wa Mazinde na
vijiji vya jirani mawasiliano ya uhakika katika kuendesha shughuli zao za
kijamii na kiuchumi kila siku ikiwemo kilimo cha katani.
Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkuu wa wilaya ya Korogwe, Hafsa Mtasiwa
alisema" tunafurahi kuwa na mnara huu wa mawasiliano kwaajili ya wakazi wa
wilaya ya mazinde ambao utasaidia kukuza biashara zao na kuinua utandawazi
kupitia simu zao za mkononi".
Aliongeza kwa kusema" mawasiliano ndio chachu ya maendeleo ya uchumi wa
jamii na ulimwengu kwa ujumla. na nimatumaini yetu kuwa huduma hii
inayozinduliwa hapa leo itachangia kwa kiasi kikubwa endeshaji wa mashamba
ya katani, kilimo, biashara mbalimbali na pia kuchagia katika kubadilisha
maisha ya wengi na kwa hilo tunapenda kuwashukuru sana Airtel ".
Kwa upande wake, Meneja mauzo wa kanda ya kaskazini, Aluta kweka amesema
kampuni yake iko mstari wa mbele katika kuhakikisha inatoa huduma za
mawasiliano za uhakika zitakazorahisisha ukuaji wa uchumi na pato la taifa.
" katika ulimwengu wa leo wa sayansi na technologia watanzania wanatakiwa
kuwezesha ili kupata fulsa zitokanazo na huduma bora za mawasiliano.
Tunaamini mnara huu hautawahakikishia wakazi wa hapa mawasiliano ya uhakika
tu bali utachangia kwa kiasi kikibwa katika kuongeza pato la taifa kwa
ujumla".
Kufatia uzinduzi huo, zaidi ya wakazi takribani 10,000 na vijiji vitatu
vitafaidika na bidhaa na huduma mbalimbali ikiwemo , huduma za intaneti,
Airtel money, yatosha na nyingine nyingi
Mkuu wa wilaya ya Korogwe,Hafsa Mtasiwa (wa pili kulia)) akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa mnara wa kampuni ya simu za mkononi Airtel Kata ya
Mazinde wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. anayeshuhudia kushoto ni Meneja wa
Kampuni ya Simu ya Airtel Kanda ya Kaskazini Aluta Kweka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...