Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel leo imemtangaza bwana Benoit Janin kuwa Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo.

Bwana Janin anachukua nafasi ya Pratap Ghose ambaye ameiongoza kampuni hiyo kwa muda wa miaka mitatu.
Uteuzi wa Janin unafatia kampuni ya Millicom kununua hisa za kampuni ya Zantel ambapo sasa itashirikiana na serikali ya Zanzibar kuhakikisha kampuni ya Zantel inakua na inaboresha huduma zake.
Benoit, ambaye ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 katika sekta ya mawasiliano katika nchi za Afrika na masoko yanayokua, alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya Tigo nchini Chad kwa muda wa miaka mitatu, ambapo aliiwezesha kuwa kampuni namba moja nchini humo.

Kabla ya kujiunga na Millicom, Benoit amefanya kazi na kampuni ya mawasiliano ya Vimpelcom kama Mkugenzi wa Biashara nchini Cambodia, huku pia akiwa ameshikilia nafasi mbalimbali za kiuongozi katika kampuni ya Orange.

Akizungumzia majukumu yake mapya, Benoit alisema anatarajia kushirikiana na wafanyakazi wa Zantel katika kuhakikisha kampuni inakua na kufikia malengo yake.‘Nina furaha kubwa kujiunga na kampuni ya Zantel na ninatarajia kushirikiana na wafanyakazi wenzangu kuongeza idadi ya wateja, pamoja na kusimamia ukuaji wa kampuni kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato’ alisema Benoit.

Kama sehemu ya majukumu yake mapya, Bwana Janin ataboresha huduma za mtandao za Zantel pamoja na kuzindua huduma za 4G hapo mwakani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...