Na Lorietha Laurence-Maelezo
Bodi ya Korosho Tanzania imeadhima kutoa asilimia 7 ya mapato yake sawa na
shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kusaidia utafiti wa zao hilo unaofanywa na kituo
cha utafiti cha Naliendele.
Akiongea wakati wa kufunga kwa mkutano wa tatu wa kimataifa uliowahusisha
wadau kutoka nchi mbalimbli duniani ,Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho
Tanzania Bw. Muhidhiri Muhidhiri amesema kuwa changamoto kubwa
wanayokabiliana nayo ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuendeshea utafiti wa zao
la korosho unaofanywa na kituo cha Naliendele na hivyo wamejipanga kwa
kuchangia kiasi cha mapoto ili kufanikisha tafiti hizo .
Muhidhiri aliongeza kuwa licha ya changamoto za ukosefu wa fedha wamepata
fursa ya kujifunza mambo mbalimbali kupitia mkutano huo ikiwemo maadhimio
ya uzalishaji bora wa zao hilo, namna ya kutatua matatizo ya magonjwa
yanayoikumba korosho,dawa asilia zitakazosaidia katika kulinda mbegu, na njia
bora ya uzalishaji.
“Mkutano ulikuwa wa kisayansi kwa kuwa umeangalia mambo ya kiutafiti na
teknolojia katika uzalishaji wa zao la korosho hivyo ninaamini baada ya hapa ni
kuanza utekelezaji wa yale tuliyoyajadili na kufanya vizuri zaidi ” alisema
Muhidhiri.
Kwa upande wa Mtafiti Mkuu wa Masuala ya korosho Prof.Peter Masawe
ameeleza kuwa mkutano huo wa wadau umewapa fursa ya kufahamu mambo
mazuri katika uboreshaji na uzalishaji wa zao la korosho katika kiwango kizuri na
kilicho bora .
Pia alibainisha kuwaTanzania ndiyo nchi yenye mtafiti anayetegemewa katika
masuala ya korosho na hivyo kupitia mkutano huo wadau wamepata fursa ya
kufahamu mambo ya msingi kama vile mbegu bora zinazozalishwa nchini ,mbegu
fupi, mbegu zinazostahimili ukame pamoja na kukopa teknolojia ya uzalishaji.
“Mkutano huu umetoa fursa kwa wadau kujua mambo muhimu kuhusu mbegu
ukizingatia Tanzania ndiyo nchi pekee barani Afrika inayozalisha mbegu bora
hivyo natumai wajumbe wataenda kutendea kazi yale yote waliyojifunza hapa
kwetu na nasisi pia tutayafaniya kazi yale tuliyoyapata kutoka kwao ” alisema
Prof Masawe.
Mkutano huo wa kimatifa wa wadau wa Korosho umefanyika kwa mara ya pili
nchini ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1997 na hivyo kuipa fursa nchi ya
kujitangaza kupitia sekta ya kitalii kwa kuwahamasisha wadau waliohudhuria
mkutano huo kutembelea sehemu za vivutio ikiwemo Bagamoyo na Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...