Baadhi ya Nyumba zikibomolewa mapema leo mchana mtaa Bwawani Manispaa ya Kinondoni,ambapo zoezi hilo linafanyika maeneo mbalimbali katika Manispaa hiyo. Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, imekusudia kuanza kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi. 
 Askari wa jeshi la Polisi wakisimamaia suala la usalama mtaa wa Bwawani wakati wa bomoa bomoa ikiendelea katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar mapema leo.
Baadhi ya wakaazi wa mtaa Bwawani Manispaa ya Kinondoni wakishuhudia bomoa bomoa inayofanyika leo katika manispaa hiyo maeneo mbali mbali ambapo Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.
 Askari wa jeshi la Polisi wakisimamaia suala la usalama mtaa wa Bwawani wakati wa bomoa bomoa ikiendelea katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar mapema leo.
 Moja ya Nyumba iliyojengwa eneo la wazi katika mtaa wa Bwawani ikibomolewa 
 Askari jeshi la polisi wakihakikisha suala la usalama katika tukio hilo
 Ubomoaji wa nyumba ukiendelea eneo la Manispaa ya Kinondoni

TAARIFA ILIYOTOLEWA JANA KUHUSIANA NA UBOMOAJI WA NYUMBA MANISPAA YA KINONDONI

Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.
 Maeneo yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi, njia za miundombinu na huduma nyinginezo za umma, mara kwa mara hutumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi hivyo kuukosesha umma manufaa yaliyokusudiwa.
Tamko Na. 6.6.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:
i. Serikali itahakikisha kwamba maeneo yote mijini yaliyotengwa kwa shughuli za umma yanatumika kwa shughuli zilizokusudiwa na yanalindwa ili yasivamiwe.
Tamko Na. 8.2.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:

ii. Serikali za mitaa zitawajibika kushirikiana na Wizara ya Ardhi kuhakikisha usimamizi mzuri wa ardhi katika maeneo yao.

Sera ya Taifa ya Ardhi imebainisha sababu inayopelekea Wizara kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi hili la ubomoaji.

Ubomoaji huu utahusisha nyumba zote zilizojengwa
  a)     Bila kibali cha ujenzi
  b)     Bila kufuata michoro ya mipango miji
  c)      Bila kufuata matumizi ya ardhi (maeneo ya wazi)
Zoezi hili la ubomoaji litaendeshwa na Manispaa ya kinondoni na Wizara ya Ardhi itasimamia sera za ardhi na taratibu za uendelezaji kuhakikisha zinafuatwa na kila mmiliki wa ardhi.
Maeneo ambayo ujenzi wake umekiuka matumizi kusudiwa na yatahusika na ubomoaji huu ni  Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni – Biafra. Kazi hii inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia jumatano tarehe 18/11/2015 hadi ijumaa tarehe 20/11/2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. The mdudu, asantenii sana hapa kazi tu mchezo mchezo na mtu au watu hakuna tena kwanini tusiwe na bustani za mapumziko kwenye JIJI hili la DAR hongera Rais wetu Magufuli na serikali kwa ujumla pigeni kazi because we need new Tanzania mimi ningeomba muweke number zenu hapa viongozi wetu huko nyumbani ili na sisi tulio huku UGAIBUNI tutoe michango yetu ya mawazo endelevu ndugu zangu tunaipenda Tanzania yetu

    ReplyDelete
  2. Wasiishie kubomoa. Wawakamate baadhi ya viongozi wa ardhi walioshindwa kusimamia sheria hadi nyumba zikajengwa. Walikuwa wapi? Hao ndio wakamatwe.

    ReplyDelete
  3. Asante Rais wetu . Naamini kazi uliyoianza itaendelea katika maeneo yote ya jiji. Tafadhali njoo tabata, segerea, kimanga, Mawes na kisukuru nako tunakusubiri. Bwana akutangulie katika kazi za Kong.

    ReplyDelete
  4. Nilifikiri Ujamaa unathamini Utu Zaidi kumbe nipropaganda tu!

    ReplyDelete
  5. The mdudu, acha kutoa mapovu hakuna utu mbele ya uhalibifu utakua ni mmoja wapo sibule na bado mtatia akili chezea rais wetu Magufuli #hapakazitu kujuana kando #ukitakakumuanyaniusmwangalieusoni

    ReplyDelete
  6. NA HUKO BWAWANI WENYE PESA WAMEJENGA KWENYE MABWAWA YA MAJI NA WAMEZIBA MIFEREJI HIVYO MVUA KIDOGO TU HAPAPITI BARABARANI, NAOMBA BOMOABOMOA IFIKE MPAKA MAENEO YA KWA RUDO HAPOHAPO BWAWANI, SIKU HIZI NI MAJANGA MATUPU MVUA IKINYESHA MCHANA UNAWAZA USIKU UTARUDIJE MAJUMBANI. NAOMBA SANA ZOEZI HILI LIFIKE HAPO MAENEO YA KWA RUDO

    ReplyDelete
  7. Tunawajuwa wengi waliojenga kwenye maeneo yaliotengwa kwa plan za nchi lkn kwa kipato chao bado wapo na wanaobomolewa ni wale wanyonge

    ReplyDelete
  8. Mnashangilia hili swala hayaja wakuta Na mkae ivyoivyo yasiwakute ila kiukweli hii sio democrasia unafikili kwa hali panya road wataisha Namfumuko Wa panya road ulifumuka baada ya kuvunja kota za magomeni nasasa wanaendeleza zoezi pasipo kuwatafutia watu makazi.wengi wao waliobomolewa ilitakiwa wawaambie maana wengi sio wenye Nyumba no wapangaji ambao hawajui lolote mungu wasaidie

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...