Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana Zidikheri Mundeme amewataka wadau wa zao la pamba kuwalinda wakulima wadogo wa zao hilo kwa kuwapatia mbegu bora na madawa sahihi ili kuboresha zao hilo.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa zao hilo kutoka Kenya, Brazili na vituo mbalimbali vya utafiti vya hapa nchini uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya White sand hivi karibuni,Bwana Mundeme amesema kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa nguvu za ziada zinahitajika katika kumsaidia mkulima mdogo wa pamba hapa Tanzania.
"Kilimo cha mkataba,ukosefu wa soko na uongezaji wa thamani na kipato kidogo cha wakulima wa zao hilo ni baadhi ya changamoto zinazomkabili mkulima mdogo wa pamba ambapo mkutano huu unatakiwa kuzitafutia utatuzi changamoto hizo" aliongeza Bwana Mundeme.
Aidha amevipongeza vituo vya utafiti vya Kanda ya Ziwa kikiwemo kituo cha utafiti Ukiriguru ambacho kilitafiti mbegu mpya ya pamba aina ya UKM 08 ambayo imekuwa ikifanya vizuri sana kwa wakulima.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana Zidikheri Mundeme akihutubia wadau wa pamba (hawapo pichani) hivi karibuni katika ukumbi wa hoteli ya whatesand ilioko Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana Zidikheri Mundeme akisalimiana na wadu wa pamba baada ya kumaliza hotuba yake ilyohusu mikakati ya kuimarisha kilimo cha pamba hapa nchini.
HAYA MAMBO YA USHIRIKA YAFUTWE NDIO YANAYOWARUDISHA NYUMA WAKULIMA
ReplyDelete