Mnamo
tarehe 08/11/2015 Magazeti ya Mzalendo na Majira yaliandika habari
zilizolenga upotoshaji na taharuki kwa
wananchi na hususani watumiaji wa Maji kwa mkoa wa Dar es salaam wanaohudumiwa
na DAWASCO.
Katika
gazeti la Mzalendo lilikuwa na kichwa cha habari “Wengi Dar watumia maji yenye kinyesi” na upande wa gazeti la Majira
lilibeba kichwa cha habari “Maji machafu
yaathiri Dar”. Ndani ya habari hizo waandishi wameelezea shirika la
Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) kama moja ya chanzo cha ugonjwa wa
kipindupindu kwa kuwa maji hayo yameathirika na kinyesi.
Gazeti la Majira 08/11/2015 ukurasa wa 3
inanukuliwa “Kwa kiasi kikubwa Maji ya jiji yamekuwa yameathirika na kinyesi
cha binadamu”. mwisho wa kunukuu. Aidha nukuu nyingine kwenye gazeti la Majira
inasomeka “Wananchi wa jiji la Dar es salaam wamekuwa wakipata Majisafi na
salama kutoka mamlaka ya Majisafi na salama (DAWASCO) kwa aslimia 30 tu”.
Ikumbukwe
pia maeneo makubwa ambayo wagonjwa wa kipindupindu wanatoka ni maeneo
ambayo yameathirika na wizi wa maji kwa kiasi kikubwa na mapambano hayo bado
yanaendelea kuhakikisha wizi wa maji unakwisha maeneo hayo ni pamoja na Manzese, Buguruni ,Kigogo , Mburahati ,
Kinondoni mkwajuni pamoja na Tandale.Jitihada
zilizofanywa na Dawasco katika kudhibiti
ugonjwa huu hususa ni watumiaji Maji
ni pamoja na
Kupeleka
huduma ya maji BURE kwa maeneo
yaliyoathirika zaidi na mlipuko huo kupitia utarartibu wa Manispaa uliowekwa.
·
Kutoa
Elimu kwa wananchi kupitia vyombo vya habari , machapisho, pamoja na vikao vya
pamoja na watendaji wa Mitaa, Bwana Afya kwa maeneo yaliyoadhirika.
·
Kuanza
kwa usajili rasmi wa magari yanayofanya biashara ya maji (water bowsers) ili
kulinda afya ya mtumiaji. Zoezi lilianza
tarehe 01 October 2015 na idadi ya Magari 120 yameshasajiliwa hadi sasa.
Kuondoa
maunganisho yasiyo halali ambayo yanafanywa na baadhi ya wananchi “vishoka” , ambayo yanapeleka huduma ya
Maji kwa baadhi ya maeneo yanayoadhirika zaidi.
Dawasco
inasikitika kwa taarifa hizo za upotoshaji kwani tangu kuibuka kwa ugonjwa wa
Kipindupindu jitahada mbali mbali zimefanyika kwa kushirikiana na Mamlaka
husika ikiwemo Wizara ya Afya , Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa ,kikosi
cha kupambana na ugonjwa wa kipindupindu katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa na taaisi
nyingine nyingi zenye kutetea ustawi wa Afya ya Jamii.
Dawasco inapenda kuwakumbusha vyombo
vya habari kuzingatia weledi na utashi katika kuteleza majukumu yao ya kila
siku ili kuwapatia wananchi taarifa zilizo sahihi na zenye ukweli siku zote.
Tunaamini
kosa la namna hiyo halitajirudia tena ili kuepusha adha na usumbufu kwa
wananchi kama ulivyojitokeza kipindi hiki.
“Dawasco
mbele kwa mbele”
Bi
Everlasting Lyaro
Kaimu
Meneja Uhusiano - Dawasco
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...