Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Shaaban Ntarambe akiongea na watendaji na maafisa ugani wa Tarafa ya Kachwamba.

Na Richard Bagolele- Chato.

Mkuu wa Wilaya ya Chato Bw. Shaaban Ntarambe amesema wataalamu wa kilimo vijijini wanao wajibu mkubwa katika kuhakikisha uzalishaji wa mazao ya chakula na Biashara unaongezeka na kukidhi mahitaji ya jamii na masoko.

Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kilimo wilayani hapa ziara ambayo ameifanya kwenye tarafa zote tano ambapo ziara hiyo pia ilikuwa na lengo la kujitambulisha kwake tangu ateuliwe kuwa mkuu wa Wilaya hiyo mwezi Otoba 2015 .

Akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mkuu wa Wilaya amewaagiza wataalamu wote wa kilimo kutokukaa ofisini na badala yake watembelee wakulima na kuwashauri juu ya kilimo bora na kanuni zake, “Najua wengi wenu mpo likizo, mubadilike kwani vigezo vya kupendana katika kazi viwe katika misingi ya kazi wasaidieni wakulima” alisema Mkuu wa Wilaya.

Mbali na kusitiza juu ya kilimo cha Pamba Mkuu wa Wilaya pia amewaagiza wataalamu hao kuhakikisha wanakuwa na mashamba ya mfano katika maeneo wanayosimamia ili iwe rahisi hata kwa wakulima kujifunza kupitia mashamba hayo. Mashamba ya mfano yaliyosisitizwa ni ya mazao yote ya msingi yanayolimwa wilayani hapa ambayo ni Mpunga, Alizeti, Mahindi na Mhogo. 

Bw. Ntarambe amewaagiza maafisa ugani wote kuhakikisha wanapima mashamba ya wakulima wote waliopo wilayani Chato ili kuwa na takwimu sahihi za eneo lililolimwa msimu wa 2015/2016.
Watendaji na maafisa ugani wa tarafa ya Buseresere wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya chato (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kuhamasisha kilimo.

Mkuu wa Wilaya pia amewaagiza wataalamu wa kilimo wanawafundishe na kuhakikisha wakulima wote wanafuata kanuni za kilimo bora ikiwa ni pamoja na matumizi ya mbolea na kupanda kwa nafasi na kusimamia usambazaji wa pembejeo za ruzuku na kuhakiksha walengwa wananufaika na mpango huo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Mhandisi Joel Hari amewataka watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya wahamiaji wanaohamia wilayani hapa ambapo amewataka kuwa na daftari maalumu la wahamiaji ili kuepuka kuwa na wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.  Amewataka watendaji na wataalamu wa ugani vijijini kubadilika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi zenye kuleta tija katika jamii. 
Watendaji na maafisa ugani wa tarafa ya Chato wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya chato (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi kuhamasisha kilimo.

Kwa upande wao wataalamu wa kilimo wameomba uongozi wa Wilaya ya Chato kuhakikisha wanatenga bajeti ya kununulia pikipiki ili ziweze kurahisisha kuwafikia wakulima. Wamesema wamekuwa wakishindwa kuwafikia wakulima walioko mbali na makazi yao kutokana na gharama za kukodi pikipiki kuwa juu.

Wamemwomba Mkurugenzi Mtendaji kuharakisha zoezi la usambazaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima ili kwenda sambamba na msimu wa kilimo.

Ziara hiyo ya siku tatu ililenga kuhamasisha shughuli za kilimo kupitia kwa maafisa ugani na watendaji wa vijiji na kata. Wilaya ya Chato inao maafisa 89 ambao wapo katika kata na vijiji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...