Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha la kumshukuru mungu kwa amani na utulivu wakati wa uchaguzi mkuu, Alex Msama akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar na kuwahusisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za kiroho kutoka ndani ya nje ya nchi. Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo, Khamis Pembe.
KANISA la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) mkoani
Akizungumza mwishoni wa wiki jijini Dar, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo,Alex Msama
alisema amepokea taarifa hiyo kutoka kwa Mchungaji wa kanisa hilo
mkoani Dodoma ,
Elia Meshack.
Msama
alisema Mchungaji Meshack ameliomba tamasha hilo
ili kufikisha asante yao kwa Mungu baada ya kufanikisha uchaguzi Mkuu wa Tanzania
uliofanyika Oktoba 25 nchini kote.
Aidha
Msama kwa kuwa waliandaa tamasha la kuombea amani uchaguzi Mkuu, hapana budi
kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kuomba amani katika uchaguzi huo.
“Nimezungumza
na Mchungaji Meshack akinieleza kwamba itakuwa vema Tamasha la Shukrani
nikilifikisha mkoani Dodoma , Kamati yangu
inafanya mikakati ya kuweza kufikisha asante kwa Mungu,” alisema Msama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...