SALAMU
ZA PONGEZI
Rais wa Ireland, Mheshimiwa Michael D.
Higgins amemtumia Salamu za Pongezi Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika Salamu zake hizo, Rais Higgins
amesema Ireland na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri na wa kirafiki kwa miaka
mingi, hivyo ana matarajio kwamba katika kipindi cha uongozi wa Rais Magufuli, uhusiano
huo utaimarishwa zaidi.
“Ireland na Tanzania zimekuwa na
mipango ya maendeleo na ushirikiano kwa miaka mingi katika nyanja za kilimo na
lishe, uimarishaji wa huduma za afya na uendelezaji wa utawala bora na
uwajibikaji”, amesema
Rais Higgins katika Salamu zake.
Aidha, amesema Ireland inavutiwa na
maendeleo ya kiuchumi na kijamii yaliyokwisha kufanywa na Tanzania katika miaka
ya karibuni, hivyo nchi hiyo itaendeleza ushirikiano wake na Mheshimiwa
Magufuli na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
20 Novemba, 2015



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...