Na Bashir Yakub
Serikali mpya imeanza kwa kasi kubwa kufuta umiliki wa viwanja nyumba na kubomoa yale maeneo yote wanayoona hayastahili. Upo umuhimu wa kujua namna ya kuepuka kuingia katika janga hili.
1.Kifungu cha 45 (2)(i-vi) cha Sheria ya Ardhi kinaeleza sababu za msingi zinazoweza kusababisha mhusika kubomolewa, kufutiwa umiliki ardhi kama ifuatavyo :
( a ) Kwanza iwapo eneo limetelekezwa kwa muda usiopungua miaka miwili. Muda usiopungua miaka miwili maana yake ni kuanzia miaka miwili na kwenda mbele. Kutelekeza eneo kwa mujibu wa maana hii hapa ni pamoja na kutoonekana ukishughulika na eneo lako kwa namna yoyote tangu upatiwe umiliki.
( b ) Jaribio lolote la kutaka kuuza au kugawa ardhi kwa mtu asiyekuwa Mtanzania. Ni kosa mtu asiyekuwa raia wa Tanzania kumiliki ardhi, hivyo jaribio lolote la kumpatia ardhi linatosha kuwa kosa la kufutiwa umiliki.
( c ) Epuka kujenga maeneo ya wazi, maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya miundo mbinu, na huduma nyingine za umma. Kufanya hivyo hutafsiriwa kama kuukosesha umma manufaa yaliyokusudiwa na ni kinyume na tamko namba 6.6.1 la sera ya taifa ya ardhi ya mwaka 1995.
( d ) Jaribio lolote la kutoa ardhi kwa mamlaka nyingine kinyume na namna ulivyoagizwa na mamlaka wakati unapewa eneo husika.
( e ) Kutumia eneo kinyume na masharti yaliyo kwenye hati ikiwa ni pamoja na matumizi yoyote yaliyo kinyume na sheria ya ardhi, sera, miongozo na kanuni zake.
( f ) Pia, Rais kwa mamlaka aliyonayo, anaweza kufuta umiliki wa ardhi ya mtu yeyote kwa sababu zozote zinazohusu maslahi ya umma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...